-
Waziri wa Utamaduni wa Iran anamuwakilishi Rais Pezeshkian katika maziko ya Papa
Apr 26, 2025 02:33Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Salehi, yuko Roma ambako anashiriki katika maziko ya aliyekuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, kwa niaba ya Rais Masoud Pezeshkian.
-
Iran yamwita balozi wa Uholanzi juu ya tuhuma 'zisizo na msingi' dhidi ya Tehran
Apr 25, 2025 23:09Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imemwita balozi wa Uholanzi kuwasilisha malalamiko makali ya Tehran dhidi ya tuhuma "zisizo na msingi" zilizotolewa na Uholanzi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Trump adai yuko tayari kukutana na Kiongozi Muadhamu wa Iran
Apr 25, 2025 23:09Rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kukutana na Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian au Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amesema hayo katika mahojiano na TIME.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Mazungumzo na Marekani yanaendelea kwa tahadhari
Apr 25, 2025 10:17Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran, Hujjatul-Islam Sayyid Mohammad Hassan Abu-Torabi Fard amesisitiza kuwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani yanafanyika kwa tahadhari na kutoka kwenye nafasi yenye nguvu na heshima.
-
Baqaei: Mashambulizi dhidi ya makazi ya muda ya wakimbizi ni mfano halisi wa uhalifu wa kivita
Apr 25, 2025 09:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali hujuma na vitendo vya kigaidi vya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na Lebanon.
-
Mpango wa nyuklia wa Iran, ajenda ya mazungumzo ya pande nne za Iran, China, Russia na Mkuu wa IAEA
Apr 24, 2025 23:44Wawakilishi wa Iran, China na Russia wamekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA na kujadili hali ya mpango wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Iran yaonya; Israel inataka 'kuvuruga diplomasia' kupitia hujuma, mauaji ya kigaidi
Apr 24, 2025 07:18Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi ameonya kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel na makundi fulani yenye maslahi maalumu huenda yakajaribu "kuvuruga diplomasia" kupitia vitendo vya hujuma na mauaji ya kigaidi wakati huu ambapo Jamhuri ya Kiislamu na Marekani zinafanya mazungumzo ya kufikia makubaliano kuhusu shughuli za nyuklia za taifa hili.
-
"Msimamo wa ujasiri wa Papa Francis dhidi ya dhulma hautasahaulika"
Apr 24, 2025 07:08Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Masuala ya Kisiasa wa Iran amesema, mchango wa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani aliyeaga dunia hivi karibuni, Papa Francis ambaye daima alikuwa mstari wa mbele kusaidia wanyonge na wahanga wa unyanyasaji na ukatili, na vile vile misimamo yake ya kijasiri dhidi ya ukandamizaji, dhulma, ubaguzi na unyanyasaji kamwe haitasahaulika.
-
China yaitaka Marekani iwe "mkweli" katika mazungumzo na Iran
Apr 24, 2025 03:59Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China ameitaka Marekani kuwa na ukweli wa kisiasa katika mazungumzo yake na Iran.
-
Iran: Vikwazo vipya ni ishara ya 'kutokuwa na nia njema' Marekani katika mazungumzo
Apr 24, 2025 00:44Iran imelaani vikali vikwazo vipya vya "haramu" ilivyowekewa na Marekani ikisisitiza kuwa vinakinzana na madai ya Washington ya kuwa na nia ya dhati ya kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu