Araqchi: Marekani imependekeza kuanza tena mazungumzo na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i128986
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi ametaka kufidiwa hasara za vita vya mwezi uliopita na kusisitiza kuwa Marekani inapasa kufidia hasara zilizosababishwa kwa Iran katika vita vya karibuni vya siku 12.
(last modified 2025-07-31T12:31:09+00:00 )
Jul 31, 2025 12:31 UTC
  • Sayyid Abbas Araqchi
    Sayyid Abbas Araqchi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi ametaka kufidiwa hasara za vita vya mwezi uliopita na kusisitiza kuwa Marekani inapasa kufidia hasara zilizosababishwa kwa Iran katika vita vya karibuni vya siku 12.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza haya katika mahojiano na jarida la Financial Times. 

Akiuliza swali kwamba, kwa nini Marekani inapasa kutoa maelezo juu ya sababu ya kuishambulia Iran katikati ya mazungumzo ya pande mbili, Sayyid Abbas Araqchi amesema: Marekani inapasa kutoa hakikisho kwamba tukio kama hilo halitatokea tena siku zijazo. 

Katika sehemu nyingiine ya mahojiano hayo, Araqchi amesema:" Mimi na Steve Witkoff, mwakilishi maalumu wa Marekani, tulibadilishana ujumbe wakati wa vita na baada ya hapo na tuliieleza Washington kwamba mgogoro wa nyuklia wa Iran unapasa kupatiwa ufumbuzi kwa njia ambayo itakuwa na maslahi kwa pande mbili. 

"Hakuna mapatano yanayoweza kufikiwa maadamu Trump anataka kusimamishwa kikamilifu urutubishaji wa urani', amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Araqchi amesema: "Tunaweza kufanya mazungumzo, wao pia wanaweza kuwasilisha hoja zao, na sisi tutawasilisha hoja zetu." 

Mkuu wa chombo cha diplomasia wa Iran amesisitiza kuwa njia ya mazungumzo ni nyembemba lakini inawezekani.