Iran yaonya kuhusu ya njama za Israel kuvuruga usalama Asia Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i129044
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa utawala wa Israel unalenga kuvuruga hali ya usalama katika ukanda wa Asia Magharibi (Mashariki ya Kati), na amezitaka nchi zote za eneo kuwa macho na kuchukua tahadhari ili kukabiliana na njama hizo.
(last modified 2025-08-02T05:52:53+00:00 )
Aug 02, 2025 04:24 UTC
  • Iran yaonya kuhusu ya njama za Israel kuvuruga usalama Asia Magharibi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa utawala wa Israel unalenga kuvuruga hali ya usalama katika ukanda wa Asia Magharibi (Mashariki ya Kati), na amezitaka nchi zote za eneo kuwa macho na kuchukua tahadhari ili kukabiliana na njama hizo.

Akizungumza kwa njia ya simu na Naibu Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan, siku ya Ijumaa, Araghchi amesema kuwa utawala wa Israel umezoea siasa za uchokozi na kukaidi sheria za kimataifa.

Wanadiplomasia hao wa ngazi za juu wa  wa Iran na UAE pia wamejadili kwa kina hali ya sasa ya kisiasa katika eneo la Asia Magharibi, hasa katika yanayojiri Palestina.

Aidha, wameathmini fursa zilizopo za kuimarisha uhusiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, na kibiashara, na wakaeleza haja ya kutumia uwezo na rasilimali za mataifa yao kukuza ushirikiano wa kimkakati katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.

Katika muktadha huo, mwezi Julai, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Ali Akbar Ahmadian, pamoja na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa UAE, Tahnoun bin Zayed Al Nahyan, walitoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja baina ya mataifa ya ukanda ili kuimarisha usalama kufuatia siku 12 za mashambulizi ya pamoja kati ya Israel na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.