Mamluki wa Saudia na Imarati watwangana Hadhramaut Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i134000-mamluki_wa_saudia_na_imarati_watwangana_hadhramaut_yemen
Muungano wa Kikabila wa Hadramaut wa vibaraka wa Saudi Arabia umeanzisha mashambulio makali dhidi ya vibaraka wa Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) ukitangaza kwamba kundi la Imarati limekanyaga makubaliano ya kusitisha vita baina yao na linahusika na mauaji yanayoendelea hivi sasa katika jimbo hilo.
(last modified 2025-12-07T02:22:27+00:00 )
Dec 07, 2025 02:22 UTC
  • Mamluki wa Saudia na Imarati watwangana Hadhramaut Yemen
    Mamluki wa Saudia na Imarati watwangana Hadhramaut Yemen

Muungano wa Kikabila wa Hadramaut wa vibaraka wa Saudi Arabia umeanzisha mashambulio makali dhidi ya vibaraka wa Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) ukitangaza kwamba kundi la Imarati limekanyaga makubaliano ya kusitisha vita baina yao na linahusika na mauaji yanayoendelea hivi sasa katika jimbo hilo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, huku vita kati ya mamluki wa Saudi Arabia na Imarati vikiendelea katika maeneo ya kusini na mashariki mwa Yemen, hasa Hadramaut, Muungano wa Kikabila wa Hadramaut unaohusishwa na Saudia umetoa taarifa ukiutaka Muungano wa Falme za Kiarabu udhibiti watu wake nchini Yemen na uheshimu makubaliano yaliyosainiwa kati ya mamluki wa Saudi Arabia na Imarati nchini humo.

Mamluki hao wa Saudia wameishutumu Imarati kwa kuendelea kuwamiminia fedha nyingi mamluki wake nchini Yemen na wamesema kuwa Imarati inahusika na mauaji yanayoendelea, uporaji na uhalifu mwingi ambao huko Hadramaut.

Muungano wa Kikabila wa Hadhramaut unaohusishwa na Saudia umesisitiza pia kwamba: Siku chache zilizopita, makubaliano yalifikiwa kati yao na uongozi wa serikali za mitaa za jimbo la Hadhramaut na kusainiwa na pande zote mbili kwa lengo la kuanzisha usitishaji mapigano na kupunguza mvutano, na pia ulijumuisha kuondolewa vikosi vya Hadhramaut vya ndani, kwenye visima vya mafuta.

Muungano wa Kikabila wa Hadhramaut umesema pia kwamba wanamgambo wanaofadhiliwa na Muungano wa Falme za Kiarabu wanaendelea kufanya jinai na mashambulizi kwa lengo la kulitumbukiza jimbo la Hadhramaut kwenye machafuko na migogoro. Umesema, hicho ni kitendo cha kihalifu na cha woga na kuwataka mamluki wa Imarati wabebe lawama za yote yanayotokea huko Hadhramaut hivi sasa.