Tarehe 16 Azar; Nembo ya utamaduni wa muqawama na harakati ya uhuru
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i134074-tarehe_16_azar_nembo_ya_utamaduni_wa_muqawama_na_harakati_ya_uhuru
Tarehe 16 mwezi Azar inayosadifiana na Disemba 7 imesajiliwa katika kalenda rasmi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni "Siku ya Mwanachuo", siku ambayo ni nembo ya mapambano, kupigania haki na kusimama kidete tabaka la wasomi dhidi ya dhulma na ubeberu wa madola ya kigeni.
(last modified 2025-12-08T11:03:16+00:00 )
Dec 08, 2025 11:01 UTC
  • Tarehe 16 Azar; Nembo ya utamaduni wa muqawama na harakati ya uhuru
    Tarehe 16 Azar; Nembo ya utamaduni wa muqawama na harakati ya uhuru

Tarehe 16 mwezi Azar inayosadifiana na Disemba 7 imesajiliwa katika kalenda rasmi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni "Siku ya Mwanachuo", siku ambayo ni nembo ya mapambano, kupigania haki na kusimama kidete tabaka la wasomi dhidi ya dhulma na ubeberu wa madola ya kigeni.

Siku hii inaadhimishwa kwa kuwakumbuka wanachuo watatu wa Chuo Kikuu cha Tehran waliouawa shahidi mwaka 1953 na inajulikana kama nembo ya ya harakati ya wanachuo katika historia ya zama hizi ya Iran. 

Tarehe 16 mwezi Azar mwaka 1332 hijria shamsia; yaani miezi minne tu baada ya mapinduzi ya tarehe 28 mwezi Mordad Chuo Kikuu cha Tehran kiligubikwa na maandamano ya wanachuo waliokuwa wakipinga ziara rasmi ya Richard Nixon (makamu wa Rais wa wakati huo wa Marekani) na kuanzishwa tena uhusiano kati ya Iran na Uingereza. Wanajeshi walivamia Chuo hicho kikuu na kuwauwa shahidi wanachuo watatu wa kitivo cha ufundi. Tukio hilo haraka likawa ishara ya mapambano ya wanachuo dhidi ya ukandamizaji ndani ya nchi na madola ajinabi. 

Richard Nixon

Siku ya Mwanachuo inakumbusha mapambano yaliyoendeshwa na wanachuo mkabala wa  serikali dhalimu na  uingiliaji wa nchi ajinabi; na imesajiliwa katika kumbukumbu ya kihistoria ya taifa la Iran kamanembo ya kupigania uhuru na ukombozi. Kila mwaka siku hii pia huwa fursa kwa ajili ya kuchunguza nafasi ya Vyuo Vikuu na wanachuo katika matukio ya kisiasa na kijamii ya nchi. Baada ya tukio hili, harakati ya wanachuo ikawa moja ya harakati muhimu za kijamii na kisiasa nchini Iran na katiika miaka iliyofuata ikawa na  nafasi kubwa katika mapambano ya wananchi.

Mchango au nafasi ya kihistoria ya Siku ya Wanachuo  inaonyesha kwamba Chuo Kikuu sio tu mahali pa elimu ya kitaaluma, lakini pia ni ngome ya ufahamu na uadilifu. Tarehe 16 Azar ni nembo ya kupinga uistikbari kwa sababu mwaka 1953, wanachuo walijitolea maisha yao kupinga uingiliaji wa Marekani na Uingereza na ukandamizaji wa utawala wa Pahlavi, na kukifanya Chuo Kikuu kuwa ngome ya mapambano dhidi ya udhibiti wa madola ajinabi na ukandamizaji wa ndani.  

Mapambano ya wanachuo dhidi ya Marekani na Uingereza

Katika kumbukumbu ya kihistoria ya Iran, tarehe 16 Azar inasalia kuwa nukta ya kuanzia harakati za kupigania haki na kupinga utawala wakiimla. Hii leo pia hafla za kuadhimisha Siku ya Mwanachuo ni fursa kwa ajili ya kuchunguza nafasi ya mwanachuo katika mapambano dhidi ya ubeberu wa kimataifa na kuhami uhuru wa kitaifa. Tarehe 16 Azar  si siku ya ukumbusho tu; bali pia ni nembo ya utamaduni wa mapambno ya ukombozi na kupigania uhuru yaliyoanzia chuo kikuu na kuenea katika jamii nzima ya Iran.

Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1357 hijria shamsia; wanachuo waliingia katika marhala mpya wakiwa na arii ile ile ya kupigania uhuru na ukombozi. Kutekwa kwa pango la kijasusi la Marekani tarehe 3 Novemba, 1979 ilikuwa ni nukta ya kilele ya harakati ya wanachuodhidi ya uistikbari; ambapo Imam Khomeini alikitaja kitendo hicho cha wanafunzi wa Chuo Kikuu wafuasi wa njia ya  Imam kuwa "Mapinduzi ya Pili." Wakati wa kipindi cha kujihami kutakatifu wanachuo pia walikuwa mstari wa mbele kupelekwa katika medani za mapambano. 

Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu; wwepo wa vuguvugu la wanafunzi uliendelea katika ari ile ile katika nyanja za kisiasa, kitamaduni na kisayansi; ambapo kutekwa pango la kijasusi  nakushiriki katika medani za kujihami kutakatifu  na kupiga hatua katika maendeleo ya kisayansi yote haya yanadhhirisha mchango mkubwa wa wanachuo  katika nyanja mbalimbali za jamii. Chuo Kikuu na wanachuo walichukua hatua sawa na dhamii iliyo macho ya jamii na walisimama ngangari dhidi ya udhalimu na ushawishi wowote wa maajinabi.