Iran yatambua majeshi ya Ulaya kama mashirika ya kigaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i136140-iran_yatambua_majeshi_ya_ulaya_kama_mashirika_ya_kigaidi
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Mohamad Bagher Ghalibaf amelitaja Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kama taasisi ya kipekee zaidi ya kupambana na ugaidi duniani, akibainisha kuwa Ulaya 'imejipiga risasi mguuni' kwa kuiweka IRGC kwenye orodha yake nyeusi.
(last modified 2026-02-01T10:21:13+00:00 )
Feb 01, 2026 10:21 UTC
  • Iran yatambua majeshi ya Ulaya kama mashirika ya kigaidi

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Mohamad Bagher Ghalibaf amelitaja Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kama taasisi ya kipekee zaidi ya kupambana na ugaidi duniani, akibainisha kuwa Ulaya 'imejipiga risasi mguuni' kwa kuiweka IRGC kwenye orodha yake nyeusi.

Akihutubia kikao cha Bunge leo Jumapili, Ghalibaf amesema hatua kama hizo dhidi ya Iran hazina matokeo mengine ghairi ya kuimarisha mshikamano wa kijamii katika kuiunga mkono IRGC ili kulinda heshima na usalama wa taifa la Iran.

Spika wa Bunge la Iran amesema, "Ningependa kutangaza hapa kwamba, kwa mujibu wa Kifungu cha 7 cha Sheria ya Hatua za Kulipiza Kisasi, na katika kujibu tangazo la IRGC kama shirika la kigaidi, majeshi ya nchi za Ulaya yatachukuliwa kuwa makundi ya kigaidi, na matokeo ya hatua hii yatabebwa na Umoja wa Ulaya." 

Spika Ghalibaf amesisitiza kuwa, Ulaya inataka kumridhisha "bwana" wake, Marekani, ili iwache kutishia mamlaka zao za kujitawala na umoja wa ardhi zao."

Ghalibaf ameashiria maadhimisho ya kumbukizi ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu uliokomesha utawala wa kibeberu juu ya Iran, akisisitiza kwamba Imam Khomeini MA alihuisha ujasiri wa taifa ambalo lilikuwa limeshuhudia uvamizi, mapinduzi yaliyoungwa mkono na maajinabi, na kupoteza maeneo ya ardhi yake chini ya serikali iliyokuwa tegemezi. Amesema mapinduzi hayo yaliwawezesha Wairani kulinda umoja wa kitaifa na uhuru na kusimama dhidi ya utengano na uingiliaji wa maajinabi.

Kabla ya hapo,  Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilitoa taarifa, ikiuita uamuzi huo wa Umoja wa Ulaya wa kutoa shutuma zisizo na msingi dhidi ya jeshi la SEPAH la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuliweka katika orodha yake ya ugaidi kuwa haramu, usio na haki, na wa udanganyifu.