Kamari kubwa ya Israel Ghaza yashindwa vibaya kwa kuangamizwa Abu Shabab
-
Kamari kubwa ya Israel Ghaza yashindwa vibaya kwa kuangamizwa Abu Shabab
Kuangamizwa kiongozi wa genge la kigaidi na mamluki wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, ni kufeli njama za kijasusi za utawala huo huko Ghaza na ni uthibitisho kwamba njama za kutafuta kundi la kuchukua nafasi ya Hamas ni kamari isiyo na mwisho.
Shirika la Habari la Tasnim limeandaa ripoti maalumu kufuatia kuangamizwa Yasser Abu Shabab, kiongozi wa genge la kigaidi ambalo ni mamluki wa utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na kuongeza kuwa, Yasser Abu Shabab ni gaidi maarufu zaidi aliyekuwa anatumiwa waziwazi na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na yeye na genge lake walifanya jinai kubwa dhidi ya wananchi wa Ghaza hasa wakati Israel ilipokuwa inafanya mauaji ya kimbari kwa muda wa miaka miwili dhidi ya wakazi wa ukanda huo.
Kuna uchambuzi mbalimbali unaendelea kutolewa kuhusu mauaji ya Abu Shabab na chanzo chake. Mwandishi wa habari Mpalestina, Thabet al-Amour amesema katika makala yake kwamba, ili kujua kwa kina mauaji ya Abu Shabab kunahitajika kujibiwa maswali haya mawili ambayo ni: Abu Shabab ameuawa vipi? Na ni nani aliyemuua?
Kwa mtanzamo wa mwandishi huyo Mpalestina, Abu Shabab huenda alivamiwa na wapiganaji wa Muqawama. Lakini pia inawezekana Wazayuni wenzake ndio waliomuua baada ya kuona hana faida tena kwao baada ya kusitishwa vita Ghaza na tatu kuna uwezekano kwamba mauaji yake yametokana na mzozo wa ndani wa genge lake la kigaidi huku kila mmoja akitaka apate manufaa makubwa zaidi ya kulisaliti kwake taifa la Palestina.
Mwandishi huyo lakini amesema kuwa, jambo lisilo na shaka ni kwamba, kuangamizwa Abu Shabab ilikuwa ni kufeli kamari ya karibuni kabisa ya Israel na si rahisi kwa wananchi wa Palestina na hasa wa Ukanda wa Ghaza kuachana na Muqawama wao, na milele wataendelea kuwahesabu wanaosaliti malengo matakatifu ya ukombozi wa Palestina kuwa ni wasaliti wakubwa.