Qalibaf amwambia Spika wa Knesset: Nyinyi ni aibu kwa ubinadamu
-
Mohammad Baqir Qalibaf
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameandika katika ujumbe wake kwa Spika wa Knesset (Bunge la Israel) kwamba: "Ulimwengu unashuhudia mauaji makubwa zaidi ya kimbari yanayofanywa na Israel. Nyinyi ni aibu kwa ubinadamu."
Mohammad Baqir Qalibaf ameandika katika ujumbe wa X akimjibu spika wa Bunge la Israel ambaye ametaja matamshi yake kuwa ni ya uwongo akisema: "Spika mtendajinai wa Knesset anadai kuwa njaa ya watoto wa Gaza ni 'habari za uongo.'
Spika wa Bunge la Iran ameongeza kusema: "Ulimwengu unashuhudia mauaji makubwa zaidi ya kimbari katika historia mnayoyafanya sasa. Je, wataalamu wa UN, UNICEF na mashirika ya misaada wanadanganya, na ninyi tu ndio mnasema ukweli? Nyinyi ni aibu kwa binadamu."
Katika ujumbe wake huo, Qalibaf ametaja ripoti nne za hivi karibuni za mashirika ya Umoja wa Mataifa ili kufichua uongo wa Spika wa Bunge la Israel ikiwemo ripoti rasmi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu ambayo imesema waziwazi kuwa: "Nchi za dunia zinakabiliwa na chaguo muhimu: Ama kukomesha mauaji ya kimbari yanayoendelea sasa au kushuhudia mwisho wa maisha ya watu huko Gaza."

Spika wa Bunge la Iran pia ameashiria ripoti ya Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, Bibi Francesca Albanese, iliyopewa jina la "Anatomy of Genocide," inayothibitisha kutokea mauaji ya kimbari na njaa ya makusudi huko Gaza.