Trump akasirishwa na matamshi ya Medvedev
Akijibu indhari iliyotolewa hivi karibuni na rais wa zamani wa Russia kwa White House, Rais wa Marekani amesema kuwa: " Mwambie Medvedev achunge maneno yake".
Rais Donald Trump wa Marekani ametuma ujumbe katika mtandao wake wa kijamii, Truth Social, akimlenga Dmitry Medvedev rais wa zamani wa Russia ambaye kwa sasa ni Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia.
Trump ameandika kuwa: Kwangu mimi sijali India na Russia zinafanya nini. Si muhimu kwangu kwamba nchi hizo zinaweza kuharibu uchumi wa wananchi wao. Tumekuwa na biashara ya kiwango cha chini sana na India, ushuru wao ni wa juu sana, ni ni miongoni mwa ushuru wa juu zaidi duniani.
Hivi karibuni Medvedev aliitahadharisha Marekani akisema kuwa: Rais Donald Trump ambaye anaitishia Moscow na wakati huo huo anazungumzia kupunguza muda wa kutatua mgogoro wa Ukraine, asisahau kuwa onyo lolote la mwisho ni hatua kuelekea katika vita na Marekani.