-
Iran: Haitatokea katu kufanywa mazungumzo ya kuufumua mpango wetu wa nyuklia
Mar 09, 2025 23:38Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa imetangaza kwamba ikiwa lengo la kutaka kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ni "kuufumua mpango wa amani wa nyuklia wa Iran," mazungumzo kama hayo hayatafanyika katu.
-
Qalibaf: Iran haitasubiri barua yoyote kutoka Marekani
Mar 09, 2025 07:57Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema Jamhuri ya Kiislamu haisubiri barua yoyote kutoka kwa Marekani, kwani taifa hili linategemea uwezo wa ndani katika kukabiliana na changamoto zake.
-
Mkuu wa AEOI: IAEA iache kufanya mambo kisiasa kuhusiana na kadhia ya nyuklia ya Iran
Mar 09, 2025 07:55Mohammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran AEOI, ameushauri Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, IAEA uache kutumia utashi wa kisiasa katika kadhia ya nyuklia la Iran.
-
Iran: Machafuko nchini Syria ni kwa manufaa ya Israel
Mar 09, 2025 03:17Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, machafuko na ukosefu wa utulivu nchini Syria ni kwa manufaa ya utawala wa Kizayuni na kwamba magenge ya kigaidi na yenye misimamo mikali yanatumia vibaya fursa hiyo kwa manufaa yao binafsi.
-
Siku ya Wanawake; Iran yataka Israel itimuliwe UN + Picha
Mar 09, 2025 03:16Ofisi ya Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa imetaka utawala wa Kizayuni utimuliwe kutoka kwenye umoja huo kutokana na jinai kubwa unazofanya dhidi ya wananchi wa kawaida wa Palestina hasa wanawake na watoto wadogo.
-
Kiongozi Muadhamu: Iran inakataa kabisa sisitizo la kufanya mazungumzo na madola ya kibabe
Mar 09, 2025 01:44Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyid Ali Khamenei, amesema kuwa sisitizo la baadhi ya madola ya kibabe juu ya kufanyika mazungumzo na Iran halilengi kutatua matatizo.
-
Iran: Hakuna mazungumzo na Marekani wakati kuna vitisho na vikwazo
Mar 08, 2025 07:51Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema Tehran haitashiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja kuhusu nyuklia na Marekani maadamu Washington inaendelea na vikwazo vya upande mmoja na vitisho.
-
Shutuma na bwabwaja za uwongo za Wamagharibi dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran
Mar 08, 2025 07:17Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: Miradi ya nyuklia ya Iran inayofanyika kwa malengo ya amani haiwezi kuangamizwa kwa shambulio la kijeshi. Araqchi ameeleza haya akijibu uropokaji na uwongo wa Wamagharibi dhidi ya miradi ya nyuklia ya nchi hii.
-
Araghchi: Kuundwa nchi moja ya kidemokrasia ndiyo suluhu ya kadhia ya Palestina
Mar 08, 2025 03:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesisitiza tena msimamo wa Tehran wa kupinga eti 'suluhisho la mataifa mawili' kuwa njia ya kupata haki za Wapalestina na kusisitiza kwamba, uungaji mkono usioyumba wa Iran kwa kadhia ya Palestina bado upo thabiti.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Mazungumzo na Marekani ni kujidhalilisha
Mar 07, 2025 07:43Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa, kufanya mazungumzo na Marekani ni kujidhalilisha. Amesisitiza kuwa, taifa la Iran ni la hamasa ya Karbala na 'Ashura na kamwe halikubali kudhalilishwa.