-
Iran: Miezi 15 ya jinai za wavamizi huko Ghaza isingewezekana bila ya msaada wa Marekani na Magharibi
Jan 17, 2025 03:50Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetangaza kuwa, sambamba na kusitishwa mauaji ya kimbari huko Ghaza, jumuiya ya kimataifa inapaswa kukabiliana kwa umakini na ipasavyo uasi wa utawala wa Kizayuni katika eneo lote la Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Inabidi kuandaliwe pia uwanja wa kukamatwa, kufunguliwa mashtaka na kuadhibiwa viongozi magaidi wa utawala katili wa Israel kwa jinai za kivita.
-
Spika wa Bunge la Iran awasili Ethiopia kwa ziara rasmi
Jan 16, 2025 23:50Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amewasili Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia akiongoza ujumbe wa ngazi za juu Bunge kwa mwaliko wa Spika wa Baraza la Wawakilishi la Ethiopia.
-
Rais Pezeshkian: Tajikistan ni mshirika wa kimkakati wa Iran katika eneo
Jan 16, 2025 23:45Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Tajikistan ni miongoni mwa washirika wetu wa kistratijia katika eneo hili, na kuna uhusiano wa karibu wa ujirani baina ya nchi hizi mbili.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Muqawama wa Palestina umeilazimisha Israel kurudi nyuma
Jan 16, 2025 07:47Baada ya kutangazwa makubaliano ya usitishaji vita huko Gaza, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam Ali Khamenei ametuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii na kuandika: Subira na kusimama kidete kwa wananchi na Muqawama wa Wapalestina vimeulazimisha utawala wa Kizayuni kurudi nyuma.
-
Rais Pezeshkian: Iran iko tayari kwa mazungumzo lakini itampondaponda adui iwapo itashambuliwa
Jan 16, 2025 07:38Matamshi ya Rais Masoud Pezeshkian katika mahojiano yake na televisheni ya NBC News ya Marekani yameendelea kuakisiwa katika vyombo vya habari vya ndani, kikanda na kimataifa.
-
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu aelekea Addis Ababa, katika ziara ya kuimarisha uhusiano
Jan 16, 2025 06:25Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Mohammad Baqer Qalibaf, ameondoka mjini Tehran leo asubuhi akielekea Addis Ababa, kwa shabaha ya kuimarisha uhusiano wa pande mbili.
-
Hamas: Tunaishukuru Iran kwa operesheni zake mbili za "Ahadi ya Kweli" dhidi ya Israel
Jan 16, 2025 04:03Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Hamas amesema katika hotuba yake baada ya kufikiwa makubaliano ya usitishaji vita huko Ghaza kuwa, HAMAS inaishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuitia adabu Israel katika operesheni mbili za Ahadi ya Kweli ambazo zilisambaratisha majigambo ya utawala wa Kizayuni.
-
Russia yasisitiza umuhimu wa Mkataba wa Ushirikiano wa Kina wa Kistratejia na Iran
Jan 16, 2025 00:58Dmitry Peskov, msemaji wa Ikulu ya Kremlin (makao makuu ya urais wa Russia), Jumanne alisema kuwa Russia inatilia umuhimu mkubwa kusainiwa mkataba wa ushirikiano wa kina wa kistratejia na Iran, akibainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu muhimu sana ya safari ya Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini humo.
-
Wanafunzi wa vyuo vikuu zaidi ya 40 vya Kenya washiriki katika mashindano ya Iranolojia
Jan 15, 2025 23:08Katika jitihada za kupanua uhusiano wa kiutamaduni, kisayansi na kielimu kati ya Iran na Kenya, mashindano ya "Iranolojia" yamefanyika nchini Kenya kwa ushirikiano na vyuo vikuu zaidi ya 40.
-
Araghchi: Kwa kujiamini kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani, Iran haijawahi katu kujiondoa kwenye mazungumzo
Jan 15, 2025 08:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haijawahi kuwa mshiriki wa kujiondoa kwenye meza ya mazungumzo kutokana na kujiamini kwamba mpango wake wa nishati ya nyuklia una malengo kamili ya amani.