Rais Pezeshkian: Tajikistan ni mshirika wa kimkakati wa Iran katika eneo
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Tajikistan ni miongoni mwa washirika wetu wa kistratijia katika eneo hili, na kuna uhusiano wa karibu wa ujirani baina ya nchi hizi mbili.
Rais Pezeshkian amesema hayo akiwa mjini Dushanbe katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake Rais Emomali Rahmon wa nchi hiyo.
Sambamba na kushukuru ukarimu wa rais, serikali na watu wa Tajikistan, Daktari Pezeshkian amesema: "Uhusiano wa kihistoria, ustaarabu na lugha ya kawaida ya Kiajemi ni kina cha urafiki na udugu kati ya nchi hizo mbili."
Masoud Pezeshkian pia alisisitiza wakati wa mazunguumzo yake na Rais wa Tajikistan kwamba uhusiano kati ya Iran na Tajikistan unaweza kuimarika zaidi, na katika nyanja zote za kiuchumi, kisayansi, kitamaduni na kisiasa.
Kadhalika amesema, tumejadili matukio mengi ya kikanda, hasa kuhusu Afghanistan. Afghanistan ni nchi muhimu jirani ya Iran na Tajikistan.
Kwa upande wake Rais wa Tajikistan, Emomali Rahmon amesema katika mazungumzo yake na Rais wa Iran Masoud Pezeshkian kwamba, ushirikiano wa Iran na Tajikistan uko katika kiwango cha juu, na nchi yake inapenda ushirikiano huo.
"Ushirikiano wa nchi hizi mbili umekua katika miaka miwili hadi mitatu iliyopita. Natumai ziara yako ya siku moja itaboresha uhusiano kati ya nchi hizi mbili na itakuwa ya baraka," aliongeza.