-
Balozi wa Saudia aitwa Wizara ya Mambo ya Nje baada ya Riyadh kuwanyonga raia 6 wa Iran
Jan 02, 2025 04:17Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kibalozi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Balozi wa Saudi Arabia mjini Tehran ameitwa wizarani hapo na kukabidhiwa malalamiko ya kimmandishi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa hatua ya Saudia ya kuwanyonga raia sita wa Iran waliokuwa wamefungwa jela nchini humo, hatua ambayo imeelezwa kuwa inapingana na mwenendo wa mashirikiano ya vyombo vya mahakama yaliyopo baina ya nchi mbili.
-
Iran kufanya mazungumzo ya kufufua mapatano ya nyuklia na mataifa matatu ya Ulaya Januari 13
Jan 01, 2025 23:12Iran inakaribia kuanza tena mazungumzo yake na mataifa matatu ya Ulaya ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani (E3) baadaye mwezi huu kuhusu kufufua mapatano kuhusu mpango wake wa nyuklia.
-
Kiongozi Muadhamu amuenzi Shahidi Soleimani, asema daima alifikiria kuhuisha Muqawama
Jan 01, 2025 09:51Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesifu na kukutaja kuwa ni kwa kipekee kujitolea kwa kamanda mkuu wa Iran wa kupambana na ugaidi, Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, ambaye aliuawa mwaka 2020 akiwa pamoja na wanajihadi wenzake katika shambulio la kigaidi la ndege isiyo na rubani ya Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.
-
Gharib Abadi: Iran ni mhanga na iko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ugaidi
Jan 01, 2025 09:10Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na masuala ya kisheria na kimataifa amesema kuwa ugaidi ni tatizo linalotishia amani na utulivu wa jamii na kwamba Iran ni mhanga wa uovu huu, na daima iko mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi.
-
Kiongozi Muadhamu: Lazima tuwe wabunifu katika upashaji wetu wa habari
Jan 01, 2025 00:22Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametoa ujumbe muhimu kuhusu udharura wa kuvitumia vizuri vyombo vya habari na vya mawasiliano ya umma hasa wakati huu wa vita vya kila upande baina ya haki na batili.
-
Bashiru Ahmed Saani: Qassem Soleimani alikuwa nguzo ya mapambano dhidi ya ugaidi Asia Magharibi
Dec 31, 2024 08:34Luteni Jenerali Qassem Soleimani, mtu anayeheshimiwa na wengi kama mbunifu muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi katika eneo la Asia Magharibi, anaendelea kukumbukwa kwa nafasi yake kubwa katika kuunda mazingira ya kijiografia ya eneo hilo.
-
Rais wa Iran: Tunataraji vita na mauaji ya kimbari yatamalizika katika mwaka mpya
Dec 31, 2024 04:13Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameelezea matumaini yake kuwa dhulma, machafuko, vita na mauaji ya kimbari yatakoma katika mwaka mpya wa 2025.
-
Pezeshkian: Hatua za kivitendo za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuimarisha amani na usalama katika eneo
Dec 30, 2024 09:11Rais Masoud Pezeshkian ameeleza kuwa mtazamo na hatua za kivitendo za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni za kueneza amani na kudumisha usalama katika ukanda huu na baina ya nchi zote za Kiislamu; na ametaka kuwepo ushirikiano mkubwa zaidi kati ya Iran na Oman katika uwanja huo.
-
Araghchi asisitiza kuundwa serikali jumuishi nchini Syria
Dec 30, 2024 09:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitizia wajibu wa kuundwa serikali jumuishi nchini Syria. Sayyid Abbas Araqchi ameeleza haya leo katika kikao na waandishi wa habari hapa Tehran akiwa na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Sayyid Badr Albusaidi.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akutana na wenzake wa UAE na Oman
Dec 30, 2024 04:24Waziri wa Mambo wa Iran Abbas Araghchi na mwenzake wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Abdullah Bin Zayed Al Nahyan wamezungumzia uhusiano wa nchi mbili na matukio ya hivi karibuni katika eneo hilo.