Araghchi asisitiza kuundwa serikali jumuishi nchini Syria
(last modified Mon, 30 Dec 2024 12:39:41 GMT )
Dec 30, 2024 12:39 UTC
  • Araghchi asisitiza kuundwa serikali jumuishi nchini Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitizia wajibu wa kuundwa serikali jumuishi nchini Syria. Sayyid Abbas Araqchi ameeleza haya leo katika kikao na waandishi wa habari hapa Tehran akiwa na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Sayyid Badr Albusaidi.

Sayyid Abbas Araghhchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema katika mazungumzo hayo kwamba wamekuwa na mjadala wa kina kuhusu Syria, na wamekubaliana kuhusu kulindwa umoja wa ardhi nzima, kudumishwa mshikamano na kuheshimiwa matukufu ya kaumu madhehebu yote na kuundwa serikali jumuishi huko Syria. "Misimamo ya Iran inashabihiana sana na ya Oman na ya aghalabu ya nchi za ukanda huu; na sote tunataka kuona amani na ututulivuu unatawala nchini Syria.  

Araqchi ameongeza kuwa: Iran na Oman zina mitazamo ya karibu kuhusu masuala ya kikanda na tunaendeleza mashauriano baina yetu. Tunaamini kuwa usitishaji vita unapaswa kutekelezwa haraka iwezekanavyo huko Ghaza ili kufunguliwa njia za kuwafikishia misaada ya kibinadamu, wananchi wa ukanda huo. 

Vilevile, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria hatua nzuri zilizopigwa hadi sasa na kusema kuwa kiwango cha mauzo ya kibiashara katika mwaka huu wa 2024 kimeongezeka mara tatu ikilinganishwa na mwaka 2019; ambapo mwaka jana 2023, biashara kati ya pande mbili ilikuwa ya thamani ya dola bilioni 2.5.  

Kwa mujibu wa mtandao wa Sahab, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Sayyid Badr Albusaidi, leo asubuhi amewasili hapa Tehran akiongoza ujumbe wa kngazi za juu wa isiasa na kiuchumi wa nchi yake.