-
Iran yakanusha tuhuma za uongo kwamba Tehran inaingilia uchaguzi wa Marekani
Oct 05, 2024 00:47Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekanusha tuhuma zinazodai kuwa Iran inaingilia uchaguzi wa rais wa Marekani, na kusema serikali ya nchi hiyo haina mamlaka ya kutoa tuhuma kama hizo.
-
Madai ya madola ya Ulaya kuhusu kutaka amani sambamba na kuunga mkono jinai za Israel
Oct 04, 2024 23:05Jibu halali la kijeshi la Iran dhidi ya vitendo vya kigaidi na kichokozi vya utawala ghasibu wa Israel liyafanya mataifa ya Ulaya kuhaha na sasa yanadai kuwa ni wapigania amani.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Usitishaji vita Lebanon na Gaza unapaswa kufanyika kwa wakati mmoja
Oct 04, 2024 23:04Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Iran inaunga mkono usitishaji vita kwa sharti kwamba, haki za wananchi wa Lebanon ziheshimiwe na kukubaliwa na Muqawama na kusema: Usitishaji huo wa mapigano unapaswa kuwa sawia na usitishaji vita huko Gaza.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Adhabu uliyopewa utawala wa Kizayuni na vikosi vya ulinzi vya Iran ilikuwa halali na ya kisheria
Oct 04, 2024 08:51Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema katika khutba za Sala ya Ijumaa ya leo kwamba, kwa kuzingatia kanuni za kiulinzi za Uislamu, Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu na sheria za kimataifa, kazi adhimu na ya kiustadi iliyofanywa na vikosi vya ulinzi vya Iran ya kuuadhibu utawala mnyonyaji damu wa Kizayuni ilikuwa halali kabisa na ya kisheria.
-
Sisitizo la Iran la kuweko mshikamano wa Kiislamu dhidi ya Israel
Oct 04, 2024 08:36Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya ulazima wa kuweko umoja na mshikamano wa Waislamu dhidi ya utawala mtendaji jinai na dhalimu wa Kizayuni wa Israel.
-
Onyo la Iran kwa waungaji mkono wa Israel; Kaeni mbali na vita
Oct 04, 2024 04:22Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amezionya nchi za Magharibi na waungaji mkono wengine wa Israel katika eneo dhidi ya kuingilia mzozo kati ya Jamhuri ya Kiislamu na utawala wa Kizayuni.
-
Iran yakosoa 'hujuma' ya Israel dhidi ya Katibu Mkuu wa UN
Oct 04, 2024 03:42Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa vikali hatua ya karibuni ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
-
Rais wa Iran: Jamhuri ya Kiislamu inapambana na vitendo vya kuhatarisha usalama na kuzusha machafuko katika eneo hili
Oct 03, 2024 22:56Rais wa Iran amesisitiza kuwa, iwapo utawala wa Kizayuni utafanya kosa lolote la kijinai, basi utakumbwa na jibu madhubuti na kali na kwamba Jamhuri ya Kiislamu inapambana na vitendo vya utawala ghasibu wa Kizayuni vya kuzusha machafuko na kueneza mgogoro katika eneo hili.
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: G-7 itumie nyenzo zake kukomesha mauaji ya kimbari ya Wapalestina
Oct 03, 2024 22:54Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kuwa kundi la G-7 linapasa kutumia nyenzo zake za mashinikizo ili kusitisha haraka mauaji ya kimbari ya Wapalestina na kukomesha mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Palestina, Lebanon, Syria na katika nchi nyingine za eneo hili.
-
Rais Pezeshkian: Iran itatoa jibu kali zaidi iwapo Israel itafanya 'kosa'
Oct 03, 2024 09:26Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema Iran bila ya shaka itatoa jibu lenye "nguvu na la kukandamiza zaidi" kwa utawala haramu wa Israel ukiwa utafanya hata kosa "dogo" tu la kujaribu kujibu shambulizi kulipiza kisasi lililofanywa Jumanne usiku na Iran kwa kuyatwanga kwa makombora maeneo nyeti ya kijeshi na kiusalama ya utawala wa Kizayuni.