-
Kan'ani: Marekani ndiyo inayopaswa kubeba dhima ya jinai za Israel huko Palestina, Lebanon na Syria
Sep 21, 2024 23:29Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya ya Iran amesema kuwa, Marekani ndiyo inayopaswa kubeba dhima na kujibu malalamiko makubwa ya kimataifa kwa kushiriki kwake katika jinai za utawala wa Kizayuni huko Palestina, Lebanon na Syria.
-
Masomo tunayojifunza kutokana na kujitetea kutakatifu, miaka 36 baada ya kumalizika vita
Sep 21, 2024 22:48Miaka 36 imepita tangu kumalizika vita vya miaka 8 ambavyo utawala wa Baath wa Iraq uliitwisha Iran, vita ambavyo vimeacha nyuma mafunzo na ibra nyingi zilizo wazi, 4 kati ya hizo zikiwa muhimu zaidi.
-
Kiongozi Muadhamu: Kujenga umma; somo muhimu zaidi la Mtume (SAW)
Sep 21, 2024 09:12Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza juu ya nafasi ya watu maalumu katika uundaji wa Umma wa Kiislamu na umoja wa ulimwengu wa Kiislamu na kubainisha kwamba, kwa kuundwa Umma wa Kiislamu, Waislamu kwa nguvu zao za ndani wanaweza kuondoa donda la saratani na khabithi la utawala wa Kizayuni kutoka Palestina na kusambaratisha ushawishi na uingiliaji wa mabavu wa Marekani katika eneo.
-
Abbas Araghchi: Muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni utaendelea hadi ukombozi wa Palestina
Sep 21, 2024 08:43Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, mapambano na muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni yataendelea hadi ukombozi wa wananchi wa Palestina utakapopatikana.
-
Kanani: Njia pekee ya kulinda nchi ni muqawama na kuimarisha mamlaka ya kitaifa
Sep 21, 2024 08:43Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, kujihami kutakatifu kumewathibitishia Wairani kwamba, njia pekee ya kulinda nchi, umoja wa ardhi yote na usalama wa taifa dhidi ya wavamizi na waungaji mkono wao waovu wenye sifa za shetani ni muqawama na kuimarisha mamlaka ya kitaifa.
-
Rais wa Iran: Hakuna shetani aliye na ujasiri wa kuishambulia Iran
Sep 21, 2024 04:42Rais wa Jamhuri ya Iran amesema kuwa, shetani yeyote hawezi kuthubutu kuivamia kijeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokan na nguvu na uwezo wake mkubwa wa kijeshi wa kumzuia adui.
-
Iran yalaani shambulizi la hivi karibuni zaidi la kigaidi la Israel nchini Lebanon
Sep 21, 2024 04:09Iran imelaani vikali shambulio la hivi karibuni la kigaidi la utawala haramu wa Israel dhidi ya jengo la makazi katika eneo lenye wakazi wengi huko Beirut, Lebanon, ambalo limesababisha maafa na kujeruhiwa watu wengi, wakiwemo wanawake na watoto.
-
Ulazima wa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura kwa ajili ya kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni
Sep 21, 2024 03:52Jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Gaza na Lebanon zinaendelea katika kivuli cha kushindwa jamii ya kimataifa kusimamisha jinai hizo.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran asisitiza umuhimu wa umoja wa Waislamu
Sep 20, 2024 09:13Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ametilia mkazo umuhimu wa kuimarishwa umoja na mshimakamano baina ya Waislamu kote duniani na kujiepusha na jambo lolote linaloibua hitilafu na mifarakano baina ya wafuasi wa dini hiyo.
-
Rais wa Iran atembelea majeruhi wa shambulio la kigaidi la Israel katika Hospitali ya Farabi, Tehran
Sep 20, 2024 09:13Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatembelea majeruhi wa shambulio la hivi karibuni la kigaidi la utawala wa Kizayuni wa Israel waliohamishiwa Iran kwa ajili ya matibabu.