-
Msisitizo wa Iran wa kuondoka bila masharti Marekani kutoka Syria
Jun 26, 2024 03:28Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, ni jambo la dharura kwa vikosi vya Marekani kuondoka kikamilifu, kwa haraka na bila masharti kutoka Syria na kwamba, hatua hiyo ni muhimu kwa ajili ya amani na utulivu wa nchi hiiyo ya Kiarabu.
-
Tehran, mwenyeji wa Jumuiya ya Mazungumzo ya Ushirikiano wa Asia (ACD).
Jun 25, 2024 22:47Kikao cha 19 cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Mazungumzo ya Ushirikiano wa Asia (ACD) kilifanyika Jumatatu hapa mjini Tehran chini ya uenyekiti wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kiongozi Muadhamu: Ushiriki mkubwa katika uchaguzi ni fahari kwa Iran, kiwewe kwa maadui
Jun 25, 2024 10:04Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema ushiriki mkubwa zaidi katika uchaguzi wa rais wa kabla ya wakati unatazamiwa kufanyika Juni 28, utalipa fahari taifa la Iran na kuwaghadhabisha maadui wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Kiongozi Muadhamu akutana na wananchi katika sherehe za Sikukuu ya Eid Ghadir Khum
Jun 25, 2024 04:31Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo amekutana na kuzungumza na maelfu ya wananchi katika sherehe ya maadhimisho ya Sikukuu ya Eid Ghadir Khum.
-
Vyombo vya habari vya nje 150 kuripoti uchaguzi wa Rais wa Iran
Jun 25, 2024 04:15Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa vyombo vya habari vya nje 150 kutoka nchi 31 vitaripoti zoezi la uchaguzi wa rais wa Iran utaofanyika Ijumaa ijayo Juni 28.
-
FAO: Iran kuzalisha zaidi ya tani milioni 20 za nafaka
Jun 25, 2024 04:15Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza kuwa, uzalishaji wa nafaka katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utazidi tani milioni 20 mwaka huu.
-
Bagheri Kani: Iran ina azma ya kuendeleza sera za ujirani za Ebrahim Raisi
Jun 24, 2024 22:59Mwakilishi maalumu wa Sultan wa Oman ambaye yuko hapa Tehran kushiriki katika mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jukwaa la Mazungumzo ya Ushirikiano wa Asia yaani Asia Cooperation Dialogue (ACD) amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran pambizoni mwa mkutano huo.
-
Mokhber: ACD inaweza kuwa na mchango muhimu katika kuasisi Asia yenye umoja, nguvu na athirifu zaidi
Jun 24, 2024 08:00Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe katika Jukwaa la Mazungumzo ya Ushirikiano wa Asia yaani Asia Cooperation Dialogue (ACD) la kundi la D-8 hapa njini Tehran kwamba Asia inaweza kuwa chanzo cha mabadiliko chanya katika michakato ya kimataifa na kichocheo kikubwa cha umoja na mshikamano wa kimataifa.
-
Iran yaalani mashambulizi ya kigaidi katika Jamhuri ya Dagestan, Russia
Jun 24, 2024 07:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyojiri katika Jamhuri ya Dagestan na kutoa mkono wa pole kwa taifa la Russia na serikali ya nchi hiyo khususan familia za wahanga wa jinai hiyo.
-
Makubaliano ya kuanzisha mazungumzo kati ya Tehran na Manama, ishara ya mafanikio ya siasa za nje za Iran
Jun 24, 2024 07:33Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Bahrain zimetoa taarifa ya pamoja zikielezea kuwekwa mikakati muhimu ya kuanzisha mazungumzo baina ya nchi mbili kwa lengo la kuchunguza namna ya kurejesha uhusiano wa kisiasa. Taarifa hii ya pamoja imetolewa kufuatia mazungumzo yaliyofanyika karibuni kati ya Ali Bagheri Kani, Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri mwenzake wa Mashauri ya Kigeni wa Bahrain.