Rais wa Iran kushiriki mkutano wa BRICS nchini Russia
(last modified 2024-08-31T13:05:24+00:00 )
Aug 31, 2024 13:05 UTC
  • Rais wa Iran kushiriki mkutano wa BRICS nchini Russia

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian anatazamiwa kushiriki Mkutano wa BRICS wa 2024 nchini Russia karibuni hivi.

Mkutano wa kwanza wa kilele wa wanachama wa BRICS baada ya upanuzi wa shirika hilo la kiserikali utafanyika mjini Kazan nchini Russia mwishoni mwa Oktoba.

Dakta Pezeshkian atashiriki katika mkutano hiyo kwa mwaliko rasmi wa Ikulu ya Russia ya Kremlin. Balozi wa Iran huko Kazan, Davoud Mirzakhani amefanya mkutano na msaidizi wa rais wa Jamhuri ya Tatarstan katika mji wa magharibi mwa Urusi ili kufanya mipango ya mkutano wa kilele wa BRICS.

Russia imechukua urais wa zamu wa BRICS mwaka huu. Iran, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Ethiopia ndizo wanachama wapya watano ambao walikua wanachama kamili wa BRICS mwanzoni mwa 2024.

BRICS ilianzishwa mwaka 2006 na awali ilijumuisha Brazil, Russia, India na China. Wanachama wapya wa jumuiya hiyo ni pamoja na Iran, Misri, Ethiopia na Umoja wa Falme za Kiarabu. Nchi nyingi zikiwemo za Afrika zimetuma maombi ya kujiunga na jumuiya hiyo.

Mkutano huo ujao wa BRICS umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwezi Oktoba mwaka huu huko Kazan makao makuu ya Tatarstan nchini Russia.

Tags