-
Kamanda wa IRGC: Iran itatoa jibu kali kwa Israel kwa wakati na mahali mwafaka
Aug 05, 2024 10:17Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ameutaja utawala wa Israel kuwa ulizaliwa kutokana na ugaidi, akisema utawala huo utakuwa katika mawindo ya makosa yake wenyewe.
-
Kan'ani Chafi: Iran yalaani shambulizi la kigaidi la Al-Shabaab mjini Mogadishu
Aug 05, 2024 04:12Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Nasser Kan’ani amelaani vikali shambulio la kundi la kigaidi la Al-Shabaab mjini Mogadishu na kuomboleza na serikali ya Somalia na familia za wahanga wa shambulio hilo la kigaidi.
-
Mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na Jordan wakutana kujadili matukio ya kikanda
Aug 05, 2024 01:13Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Bagheri Kani amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi ambaye yuko katika ziara rasmi mjini Tehran huku kukiwa na ongezeko la hali ya wasiwasi na taharuki katika eneo la Asia Magharibi.
-
Pezeshkian: Kosa 'kubwa' la Israel la kumuua kigaidi Haniyah litajibiwa
Aug 04, 2024 23:54Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kitendo cha utawala wa Kizayuni wa Israel cha kumuua kigaidi Ismail Haniyah, Kiongozi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ni 'kosa kubwa' ambalo halitapita hivi hivi bila kupewa majibu.
-
Ukosoaji wa Iran kwa baadhi ya nchi za Ulaya kwa kuunga mkono vitendo vya kigaidi vya Israel
Aug 04, 2024 23:01Ali Bagheri Kani, Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametilia mkazo haki ya kisheria ya Tehran ya kuuadhibu utawala wa Kizayuni; na amelaani na kukemea hatua ya baadhi ya nchi za Ulaya ya kushirikiana na Marekani kuzuia kulaaniwa mauaji ya Kiongozi Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) shahidi Ismail Haniyeh katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Kan'ani Chafi: Mataifa ya Kiislamu yanapaswa kutoa uungaji mkono athirifu zaidi kwa haki za Wapalestina
Aug 04, 2024 09:10Nasser Kan'ani, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran, ametoa wito kwa serikali za Kiislamu kuunga mkono haki za Wapalestina kwa ufanisi zaidi.
-
Spika Qalibaf: Jibu la Iran kwa Israel litaleta furaha kwa Wairani na vikosi vya muqawama
Aug 04, 2024 08:57Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, majibu makali na ya kiakili ya Jamhuri ya Kiislamu kwa utawala unaofanya mauaji ya kimbari wa Israel kuhusiana na mauaji ya shahidi Ismail Haniya yataleta furaha kwa watu wa Iran na vikosi vya muqawama na wapiganiia uhuru wa dunia.
-
Qalibaf: Utawala wa Kizayuni kwa mara nyingine tena umeonesha dhati yake ya kijinai
Aug 04, 2024 03:54Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, jinai za utawala wa Kizayuni katika miji ya Beirut na Tehran na kuendelea kuwaua watoto huko Ghaza, kwa mara nyingine tena zimewaonesha walimwengu dhati halisi ya kijinai, ukatili na ubeberu wa dola hilo pandikizi.
-
Uhusiano wa Tehran na Riyadh katika njia ya ustawi
Aug 03, 2024 22:55Ujumbe wa maandishi wa Mlfalme wa Saudi Arabia kwa Rais mpya wa Iran unaonyesha kuwa Saudi Arabia, kama ilivyo Iran, inataka kuimarisha na kustawisha uhusiano mpya wa pande mbili ulioanza katika kipindi cha uongozi wa Shahid Ebrahim Raisi; na kuendelea kwa uhusiano na ushirikiano huu kuna manufaa ya pande mbili.
-
Jumuiya ya Wayahudi wa Iran yataka kulipiza kisasi baada ya Israel kumuua Haniyeh
Aug 03, 2024 22:53Jumuiya ya Wayahudi wa Iran imelaani vikali mauaji yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya kiongozi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) Ismail Haniyeh akiwa ugenini mjini Tehran, ikitoa wito wa kulipiza kisasi dhidi ya mauaji hayo.