-
Spika Qalibaf: Jibu la Iran kwa Israel litaleta furaha kwa Wairani na vikosi vya muqawama
Aug 04, 2024 08:57Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, majibu makali na ya kiakili ya Jamhuri ya Kiislamu kwa utawala unaofanya mauaji ya kimbari wa Israel kuhusiana na mauaji ya shahidi Ismail Haniya yataleta furaha kwa watu wa Iran na vikosi vya muqawama na wapiganiia uhuru wa dunia.
-
Qalibaf: Utawala wa Kizayuni kwa mara nyingine tena umeonesha dhati yake ya kijinai
Aug 04, 2024 03:54Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, jinai za utawala wa Kizayuni katika miji ya Beirut na Tehran na kuendelea kuwaua watoto huko Ghaza, kwa mara nyingine tena zimewaonesha walimwengu dhati halisi ya kijinai, ukatili na ubeberu wa dola hilo pandikizi.
-
Uhusiano wa Tehran na Riyadh katika njia ya ustawi
Aug 03, 2024 22:55Ujumbe wa maandishi wa Mlfalme wa Saudi Arabia kwa Rais mpya wa Iran unaonyesha kuwa Saudi Arabia, kama ilivyo Iran, inataka kuimarisha na kustawisha uhusiano mpya wa pande mbili ulioanza katika kipindi cha uongozi wa Shahid Ebrahim Raisi; na kuendelea kwa uhusiano na ushirikiano huu kuna manufaa ya pande mbili.
-
Jumuiya ya Wayahudi wa Iran yataka kulipiza kisasi baada ya Israel kumuua Haniyeh
Aug 03, 2024 22:53Jumuiya ya Wayahudi wa Iran imelaani vikali mauaji yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya kiongozi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) Ismail Haniyeh akiwa ugenini mjini Tehran, ikitoa wito wa kulipiza kisasi dhidi ya mauaji hayo.
-
Jeshi la SEPAH latoa taarifa kuhusu kuuawa shahidi Ismail Haniya
Aug 03, 2024 10:09Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) limetoa taarifa nambari tatu inayoeleza na kubainisha jinsi Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS alivyouawa hapa mjini Tehran.
-
Iran: Kimbunga cha hasira za wapenda haki kitaukumba utawala wa Kizayuni wa Israel karibuni hivi
Aug 03, 2024 07:24Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amezungumzia jinsi utawala wa Kizayuni unavyoendelea na jinai zake na kusema kuwa, karibuni hivi utawala huo dhalimu utakumbwa na kimbunga cha hasira za mataifa na tawala zinazopenda haki na uadilifu duniani.
-
Iran yaishukuru Algeria kwa kuiunga mkono katika mkutano wa Baraza la Usalama
Aug 03, 2024 07:23Ali Bagheri, Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria, Ahmed Ataf kuhusiana na matokeo ya kitendo cha kigaidi cha utawala wa Kizayuni cha kumuua shahidi Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Hamas na kuishukuru Algiers kwa uungaji mkono wake kwa kadhia ya Palestina.
-
Baada ya UN, Iran yaitaarifu EU: Tutalitia adabu genge la wahalifu la utawala wa Kizayuni wa Israel
Aug 03, 2024 03:27Iran itatumia haki yake ya asili na halali ya kuliadhibu "genge la wahalifu la Kizayuni" kwa shambulio lake la kigaidi la siku ya Jumatano iliyopita, ambalo lilipelekea kuuawa mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) Ismail Haniyeh mjini Tehran.
-
Siasa za serikali ya 14 ya Iran ni kuendeleza ushirikiano mzuri na nchi jirani na za dunia
Aug 03, 2024 00:50Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa siasa za serikali ya 14 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uga wa siasa za kigeni ni kuwa na maingiliano mazuri na yenye uwiano na nchi jirani na dunia nzima kwa ujumla kwa lengo la kudhamini haki na maslahi ya taifa la Iran.
-
Iran yamfahamisha Katibu Mkuu wa UN kuwa itawaadhibu 'Wazayuni wahalifu'
Aug 02, 2024 10:21Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Bagheri Kani amesisitiza "haki ya asili" ya Iran ya kujilinda na kuchukua hatua za kujibu baada ya Israel kumuua Ismail Haniyeh, mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palaestina, Hamas, mjini Tehran.