-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Jinamizi la kulipiza kisasi limeutia gizani utawala wa Kizayuni
Aug 02, 2024 10:21Imamu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema: Mauaji ya Ismail Haniyeh, mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas akiwa mjini Tehran, ni kiungo cha mwisho cha jinai zinazoendelea kufanywa na genge chafu la uhalifu na linaloendelea kuua watoto la Israel.
-
Kamanda Salami: Muqawama utalipiza kisasi cha jinai za karibuni za Israel
Aug 01, 2024 23:14Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) amesema jinai za hivi karibuni za Israel katika eneo la Asia Magharibi zimechochea moto wa ghadhabu miongoni mwa wapiganaji wa makundi ya muqawama ambao sasa wana azma thabiti ya kulipiza kisasi mkabala wa utawala wa Kizayuni.
-
Mfalme Salman atoa mwito wa kuimarishwa uhusiano wa Saudia na Iran
Aug 01, 2024 23:13Mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz Aal-Saud ametoa wito wa kuimarishwa uhusiano wa pande mbili kati ya Riyadh na Tehran.
-
Kikao cha Baraza la Usalama kuhusu kuuawa kigaidi Shahidi Haniyeh
Aug 01, 2024 23:06Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza katika kikao cha Baraza la Usalama kuhusu kuuawa kigaidi Shahidi Ismail Haniyeh Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas kuwa nafasi ya Marekani kama mshirika wa kistratijia na muungaji mkono mkuu wa utawala wa Israel katika eneo katika jinai hiyo ya kutisha haipaswi kupuuzwa.
-
Spika wa Bunge la Iran: Utawala wa Kizayuni utalipa gharama ya jinai yake
Aug 01, 2024 07:49Katika kujibu mauaji ya mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas mjini Tehran, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel utalipa gharama kubwa ya chokockoko zake katika ardhi ya Iran.
-
Utawala wa Kizayuni usubiri jibu kali kwa kumwaga damu ya Shahidi Ismail Haniyeh
Aug 01, 2024 07:15Katika tukio jipya la kuibua chokochoko katika eneo, utawala ghasibu wa Kizayuni kwa mara nyingine tena umefanya kitendo kingine cha ugaidi kwa uungwaji mkono wa Marekani, ambapo umemuua shahidi Ismail Haniyeh kiongozi wa kisiasa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) mjini Tehran.
-
Pezeshkian: Maingiliano makubwa ya kiutamaduni baina ya Iran na Tanzania ni fursa ya kipekee
Aug 01, 2024 03:13Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa maingiliano makubwa ya kiutamaduni baina ya Iran na baadhi ya maeneo ya Tanzania hasa Zanzibar, ni fursa nzuri ya kustawishwa zaidi na zaidi uhusiano wa nchi hizo mbili.
-
Iran: Hatutosita kutoa majibu makali na ya haraka kwa jinai za Israel
Aug 01, 2024 03:12Balozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Tehran italinda vilivyo haki zake kwa mujibu wa kifungu cha 51 cha hati ya Umoja wa Mataifa na haitosita kutoa majibu makali na ya haraka kwa jinai za utawala wa Kizayuni.
-
Kan'ani: Kutoguswa nchi mbalimbali na jinai za Israel kunachochea ugaidi wa dola hilo pandikizi
Aug 01, 2024 03:11Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine tena amelaani jinai iliyofanywa na Israel ya kumuua shahidi Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS hapa Tehran na kusisitiza kuwa, kimya na dharau inayooneshwa na nchi na mashirika ya kimataifa mbele ya jinai za kutisha za utawala wa Kizayuni ni sawa na kuchochea ugaidi wa kiserikali unaofanywa na dola hilo pandikizi.
-
Kiongozi wa Mapinduzi kuongoza Sala ya Maiti ya kumsalia Shahidi Haniya, Iran yamuomboleza kwa siku tatu
Jul 31, 2024 23:49Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imetangaza kuwa, Ayatullah Khamenei leo asubuhi ataongoza Sala ya Maiti ya kumsalia Shahidi Ismail Haniya, Mwanjihadi mkubwa wa Muqawama wa Palestina, itakayosaliwa katika Chuo Kikuu cha Tehran.