-
Araghchi: Mazungumzo maana yake ni mazungumzo, si ukidteta; Marekani ijirekebishe kwanza
Nov 28, 2025 06:33Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Tehran itaendelea kuwa muwazi kuhusu mazungumzo, na msimamo wake utaendelea kuwa ule ule kwamba mazungumzo maana yake ni mazungumzo, si udikteta. Inaweza kufikiria kufanya mazungumzo na Marekani, lakini tu ikiwa Washington itabadilika na kuacha madai yake yasiyo na mantiki. Iingie kwenye mazungumzo ya kuheshimiana na ya usawa si ya kufanyiana udikteta.
-
Mwakilishi wa Iran akosoa undumilakuwili wa UN
Nov 28, 2025 06:33Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na jamii za wachache amekosoa misimamo ya nyuso mbili na ya kindulimakuwili la Umoja wa Mataifa katika kuyaendea masuala mbalimbali duniani ambayo yanapingwa na madola ya kibeberu.
-
Silaha za mauaji ya halaiki na sera za undumilakuwili za Washington na Tel Aviv, chanzo cha migogoro ya kiusalama Magharibi ya Asia
Nov 28, 2025 06:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Araghchi amesema, yanayoendelea kujiri katika eneo la Magharibi ya Asia ambayo ni vita vya kudumu, uchokozi wa kivamizi, mauaji ya kimbari na kujipanua kikoloni utawala wa kizayuni wa Israel, ni matokeo ya moja kwa moja ya uungaji mkono wa Marekani na uridhishaji unaofanywa na baadhi ya nchi za Ulaya kwa utawala huo haramu.
-
Kiongozi Muadhamu: Marekani haina hadhi ya kuwa na uhusiano na Iran
Nov 28, 2025 03:00Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kwenye hotuba yake kupitia televisheni ya taifa kwamba, Marekani haina hadhi ya kuwa na mahusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba vita vya siku 12 vilivyoanzishwa na Marekani na Israel ni vita vilivyopangwa kwa muda wa miaka 20 lakini taifa la Iran limeshinda na adui ameshindwa.
-
Larijani: Kuunga mkono umoja wa Umma wa Kiislamu ni mojawapo ya vipaumbele vikuu vya Iran
Nov 28, 2025 02:59Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa kulinda na kutetea umoja wa Umma wa Kiislamu ni miongoni mwa vipaumbele vikuu vya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Jeshi la Wanamaji la Iran kuzindia zana mpya za kivita
Nov 28, 2025 02:46Admeri Shahram Irani, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran, ametangaza mipango ya kuzindua vifaa vipya na kuunganisha meli mpya katika jeshi hilo.
-
Larijani: Vita vya siku 12 ni matokeo ya njama za miaka mingi za Marekani na Wazayuni
Nov 27, 2025 06:00Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesisitiza katika mkutano na wasomi wa Pakistan kwamba vita vya siku 12 ilivyolazimishwa Iran kupigana ni matokeo ya njama kubwa za Marekani na utawala wa Kizayuni na vilipangwa miaka mingi nyuma.
-
Uhusiano wa Iran na Pakistan; kiungo cha kimkakati cha amani na utulivu katika eneo
Nov 26, 2025 16:17Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amewasili Islamabad na kukutana na kushauriana na maafisa wa Pakistan katika ziara rasmi ya siku mbili.
-
Haaretz: Netanyahu amepelekea Israel kushindwa katika pande zote, hususan dhidi ya Iran
Nov 26, 2025 12:18"Sera za waziri mkuu Benjamin Netanyahu zimepelekea kushindwa Israel katika pande zote za kidiplomasia, kijeshi, na kimkakati, hususan dhidi ya Iran". Hayo ni kwa mujibu wa Haaretz, gazeti la Israel linalochapishwa kwa lugha ya Kiebrania.
-
Asilimia 86 ya vijiji vya Iran vimeunganishwa kwa barabara za lami
Nov 26, 2025 07:14Wizara ya Uchukuzi ya Iran imesema kuwa karibu vijiji tisa kati ya kumi hapa nchini vimeunganishwa kwa barabara za lami; hatua inayoashiria upanuzi mkubwa wa miundombinu ya vijijini nchini Iran.