-
Iran yatangaza orodha ya waliodhinishwa kugombea urais Juni 28
Jun 09, 2024 23:53Makao Makuu ya Uchaguzi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran yametangaza orodha ya mwisho ya viongozi waliodhinishwa kugombea uchaguzi wa mapema wa duru ya 14 ya urais wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Kamanda: Nchi za kigeni zina hamu ya kununua droni za Iran
Jun 09, 2024 23:52Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ni moja ya madola yenye nguvu kubwa za ndege zisizo na rubani (droni) duniani.
-
Bagheri Kani: Iran ni miongoni mwa 'wapaza sauti wakubwa zaidi' dhidi ya jinai za Israel Ghaza
Jun 09, 2024 06:33Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ni mojawapo ya nchi ambazo zimepaza "sauti kubwa zaidi" dhidi ya jinai za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel za mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
Wanawake wa Iran washika nafasi ya pili kwa kutwaa medali nane katika Mashindano ya Kurash,Asia
Jun 09, 2024 04:30Wanawake wa Iran wameshinda medali nane na kuwa washindi wa pili wa Mashindano ya Kurash ya Bara Asia.
-
Iran yalaani mauaji ya kinyama ya Israel katika kambi ya Nuseirat
Jun 09, 2024 00:25Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani jinai ya kutisha ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika kambi ya Wapalestina ya Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza.
-
Utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa wa Sistan na Baluchistan nchini Iran
Jun 08, 2024 22:48Kufunguliwa miradi mbalimbali ya maendeleo katika seka za maji, umeme na gesi katika mkoa wa Sistan na Baluchestan nchini Iran kunaonyesha azma kubwa ya serikali ya hayati Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Shahid Raisi, ya kustawisha maeneo yaliyokuwa yamebaki nyuma kimaendeleo nchini.
-
Iran: Kususia bidhaa za utawala wa Kizayuni ni hatua nyepesi zaidi lakini ndio athirifu zaidi
Jun 08, 2024 07:50Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Iran amesema, kuzisusia bidhaa za utawala wa Kizayuni wa Israel ndio hatua madhubuti na athirifu zaidi ya kukabiliana na ulegevu wa kutochukua hatua unaoonyeshwa na serikali mbalimbali duniani na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Bahrain imetuma salamu kupitia Russia za kutaka kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Iran
Jun 08, 2024 07:18Afisa mwandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Bahrain imetuma salamu kwa Tehran kupitia Russia za kutaka kurejesha uhusiano wa kawaida baada ya kusimamishwa kwa zaidi ya miaka minane.
-
Sisitizo jingine la Iran na Azerbaijan la kutekeleza makubaliano ya nchi mbili
Jun 07, 2024 23:02Katika mazungumzo yake ya simu na Kaimu Rais wa Iran, Mohammad Mokhber, sambamba na kutoa salamu za rambirambi kwa taifa la Iran kutokana na kuondokewa na Rais Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan, Ilham Aliyev, ameeleza mshikamano wake na serikali na wananchi wa Iran.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Israel imo kwenye maangamizi
Jun 07, 2024 09:25Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema, operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa imeonyesha udhaifu halisi wa utawala wa Kizayuni na imekuwa utangulizi wa kuangamizwa utawala huo.