Iran yalaani mauaji ya kinyama ya Israel katika kambi ya Nuseirat
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i112718-iran_yalaani_mauaji_ya_kinyama_ya_israel_katika_kambi_ya_nuseirat
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani jinai ya kutisha ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika kambi ya Wapalestina ya Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza.
(last modified 2024-06-09T00:25:10+00:00 )
Jun 09, 2024 00:25 UTC
  • Iran yalaani mauaji ya kinyama ya Israel katika kambi ya Nuseirat

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani jinai ya kutisha ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika kambi ya Wapalestina ya Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza.

Nasser Kanani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema jinai za kutisha zilizofanywa na Wazayuni katika mauaji ya kimbari ya mamia ya raia, watoto na wanawake wa Palestina katika kambi ya Nuseirat huko Gaza ni matokeo ya udhaifu na kuutochukua hatua serikali na asasi za kimataifa, likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika miezi minane ya jinai za kivita na ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Nasser Kan'ani Chafi amesema, kuendelea kwa mwenendo huo wa kutochukua hatua hakutokuwa na natija yoyote ghairi ya kuwahimiza wahalifu kuendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.

Mauaji ya kinyama ya Israel kkatika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat

 

Idara ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza ilitangaza jana kuwa, askari wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya "shambulio la kikatili ambalo halijawahi kushuhudiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Nuseirat" na kuua kwa umati Wapalestina 210 hadi hivi sasa na makumi ya watu kujeruhiwa mitaani.

Jeshi la Kizayuni linaendeleza uchokozi wake dhidi ya maeneo yote ya Jimbo la Kati la Deir el-Balah; na hali katika Hospitali ya Mashahidi wa Al-Aqswa ni mbaya sana.