Jun 09, 2024 08:00 UTC
  • Wanawake wa Iran washika nafasi ya pili kwa kutwaa medali nane katika Mashindano ya Kurash,Asia

Wanawake wa Iran wameshinda medali nane na kuwa washindi wa pili wa Mashindano ya Kurash ya Bara Asia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, siku ya kwanza ya Mashindano ya 13 ya Kurash Asia, ilimalizika kwa kutambulishwa wachezaji bora wa uzani tofauti katika kitengo cha wanawake katika uwanja wa Azadi Sports Complex wenye viti elfu 12,000 hapa mjini Tehran, Iran.

Timu ya taifa ya wanawake ya Iran ya Kurash Asia ilishinda medali 2 za dhahabu, 3 za fedha na 3 za shaba katika kitengo cha timu na kuwa mshindi wa pili katika Michezo ya Asia ya Tehran, Iran.

Timu ya taifa ya wanawake ya Korash imekuwa mshindi wa pili katika Mashindano ya Korash Asia

Kurash  ni aina ya mieleka ya kale iliyoanzishwa zaidi ya miaka elfu 3,500 iliyopita katika eneo la Asia ya kati hasa Uzbekistan na Tajikistan ya sasa.

Chimbuko la neno Kurash katika lugha ya Kiuzbeki linamaanisha "mieleka".

Katika vyanzo vingi vya historia ya Mashariki ya kale, Kurash inatajwa kama aina ya mashindano au burudani ya michezo ya umma.

Tags