-
Iran na Iraq zasisitizia haja ya kusimamishwa mauaji ya kimbari Gaza
Mar 13, 2024 04:16Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Iraq wametoa mwito wa kuchukua hatua zaidi hasa za kisiasa kwa ajili ya kusimamisha mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Kiongozi Muadhamu: Kilele cha istiqama ya wananchi wa Ghaza kinatokana na kuielewa na kuifanyia kazi Qur'ani Tukufu
Mar 12, 2024 23:18Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, usomaji wa Qur'ani ni sanaa takatifu na inabidi lengo lake kuu liwe ni kuwafundisha watu na jamii maana na ujumbe uliomo kwenye Qur'ani na kuandaa mazingira ya kuzingatiwa aya za Kitabu hicho Kitakatifu kama ambavyo pia kilele cha istiqama ya wananchi wa Ghaza kinatokana na kuielewa na kuifanyia kazi Qur'ani Tukufu.
-
Makamu wa Rais wa Iran ataka utawala wa Kizayuni utimuliwe kwenye kamisheni ya wanawake ya UN
Mar 12, 2024 08:10Ensiyeh Khazali, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika kikao cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Nafasi ya Mwanamke kuwa, utawala wa Kizayuni lazima utimuliwe kwenye kamisheni hiyo kutokana na jinai zake za miongo kadhaa za kuua mamilioni ya wanawake na watoto wadogo.
-
Amir Abdollahian: Palestina ni kadhia kuu katika vipaumbele vya Ulimwengu wa Kiislamu
Mar 12, 2024 04:30Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe akitoa mkono wa pongezi kwa Waislamu kwa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusema: "Kadhia ya Palestina inaongoza katika vipaumbele vya Ulimwengu wa Kiislamu."
-
Raisi: Wajibu wa wakuu wa nchi za Kiislamu ni kudumisha amani miongoni mwa Waislamu
Mar 11, 2024 23:43Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewapongeza viongozi na wananchi wa nchi za Kiislamu kwa mnasaba wa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusema kuwa, ni wajibu wa viongozi wa nchi za Kiislamu kuhimiza na kudumisha amani na undugu baina ya Waislamu.
-
Tume ya kutafuta ukweli; wenzo wa kisiasa unaotumiwa na Magharibi dhidi ya Iran
Mar 11, 2024 23:03Tume ya Umoja wa Mataifa ya kutafuta ukweli imetoa ripoti yake yenye tuhuma hewa na zisizo na msingi dhidi ya Iran, na kuonyesha kwa mara nyingine tena jinsi Wamagharibi wanaojinasibu kuwa watetezi wa haki za binadamu wanavyozitumia nyenzo za kimataifa kufikia malengo yao ya kisiasa.
-
Iran: Msaada wa kimaonyesho wa US kwa Gaza ni mchezo mchungu wa kuigiza
Mar 11, 2024 08:35Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani kile alichokitaja kuwa onyesho chungu la kipropaganda la Marekani na kueleza kuwa, hatua ya Washington ya kudai kuwapa misaada ya kibinadamu Wapalestina wa Gaza, na wakati huo huo inazuia juhudi za kimataifa za usitishaji vita katika eneo hilo lililozingirwa, ni kichekesho.
-
Kufutwa akaunti za mitandao ya kijamii za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi, kielelezo cha uhasama wa Magharibi dhidi ya uhuru wa kusema
Mar 11, 2024 00:52Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema, hatua ya Shirika la Kimarekani la "Meta" (Facebook ya zamani) ya kufuta akaunti za mitandao ya kijamii za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kielelezo cha uhasama na uadui wa Magharibi dhidi ya uhuru wa kusema na kutoa maoni.
-
Iran yasambaratisha mtandao wa Uingereza wa uhalifu wa kifedha na kamari ya intaneti
Mar 10, 2024 03:02Wizara ya Usalama ya Iran imefanikiwa kusambaratisha mtandao mkubwa wa kamari au kubeti kwa njia ya intaneti ambao ulikuwa unaendeshwa na watu wahalifu wakiwa Uingereza.
-
Iran na Oman zataka nchi za Kiislamu kuchukua hatua za kukomesha mauaji ya kimbari Gaza
Mar 09, 2024 23:20Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman zimetilia mkazo juu ya udharura wa mataifa ya Kiislamu kuchukua hatua za kukomesha mauaji ya kimbari huko katika Ukanda.