Amir Abdollahian: Palestina ni kadhia kuu katika vipaumbele vya Ulimwengu wa Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i109414-amir_abdollahian_palestina_ni_kadhia_kuu_katika_vipaumbele_vya_ulimwengu_wa_kiislamu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe akitoa mkono wa pongezi kwa Waislamu kwa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusema: "Kadhia ya Palestina inaongoza katika vipaumbele vya Ulimwengu wa Kiislamu."
(last modified 2024-03-12T04:30:22+00:00 )
Mar 12, 2024 04:30 UTC
  • Hossein Amir Abdollahian
    Hossein Amir Abdollahian

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe akitoa mkono wa pongezi kwa Waislamu kwa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusema: "Kadhia ya Palestina inaongoza katika vipaumbele vya Ulimwengu wa Kiislamu."

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Hossein Amir Abdollahian amesema katika ujumbe wake huo wa pongezi za Ramadhani kwamba matukio ya Gaza yanaonyesha kuwa, suala la Palestina ni lengo la pamoja la Waislamu na ni kadhia kuu miongoni mwa vipaumbele vya Umma wa Kiislamu. 

Amir Abdollahian amesema kuwa: Mwezi mtukufu wa Ramadhani unaweza kuwa fursa nzuri kwa nchi za Kiislamu kuchukua hatua madhubuti za kukomesha mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita wa utawala wa kibaguzi wa Israel  huko Gaza chini ya mwavuli wa umoja na mshikamano wa pande zote. 

Hossein Amir Abdollahian amesema mwishoni mwa ujumbe wake huo kuwa wanamapambano wa Palestina ndio washindi wakuu wa maidani hiyo. Leo Jumanne ni siku ya kwanza ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani hapa nchini Iran na katika nchi kadhaa za Kiislamu kama Indonesia, Malaysia, Australia, Oman, Brunei, Singapore, Iraq na Lebanon. 

Waislamu duniani kote waanza mfungo wa Ramadhani 

Saudi Arabia, Qatar, Imarati, Lebanon, Palestina, Uturuki na Waislamu wa madhehebu ya Sunni nchini Iraq zilitangaza jana Jumatatu kuwa siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.