-
Iran: Kutochukua hatua Baraza la Usalama dhidi ya jinai za Israel ni 'janga'
Feb 27, 2026 22:52Iran imelishutumu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kufumbia macho mashambulizi mabaya yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Lebanon, ambayo yanakiuka makubaliano ya kusitisha mapigano ya 2024.
-
Sera ya kikanda ya Iran: Imejikita katika kudumisha amani, utulivu na kutotegemea madola nje ya eneo
Feb 27, 2026 03:45Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Armenia kuhusu azma ya Iran ya kustawisha na kuimarisha uhusiano wa pande mbilii na majirani zake hasa Armenia.
-
Araghchi: Iran na US zinapiga hatua 'karibu zaidi kufikia mwafaka' katika baadhi ya masuala
Feb 27, 2026 00:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema duru ya karibuni ya mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana na Marekani iliyofanyika jana mjini Geneva, Uswisi ilikuwa moja ya mazungumzo bora, mazito zaidi, na marefu zaidi kuwahi kufanyika hadi sasa, na kwamba Tehran na Washington zimepiga hatua za "karibu zaidi kufikia mwafaka" katika baadhi ya masuala.
-
Araghchi: Marekani inapaswa kuacha misimamo ya kukinzana
Feb 26, 2026 02:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Araghchi amesema kwamba mafanikio ya mazungumzo yatategemea upande wa pili kuyachukuliwa kwa uzito na kujiepusha na tabia na misimamo inayokinzana.
-
Iran yapinga “uongo mkubwa” wa Marekani kuhusu kadhia ya nyuklia
Feb 26, 2026 02:43Iran imepinga vikali madai mapya ya Marekani kuhusu shughuli zake za nyuklia na makombora, pamoja na takwimu za waliouawa katika machafuko ya hivi karibuni, ikiyataja kuwa ni “msururu wa uongo mkubwa” huku ikikosoa kampeni iliyoratibiwa ya upotoshaji wa taarifa dhidi yake.
-
Iran yamuonya Trump asichukue maamuzi yanayotegemea taarifa za uongo
Feb 26, 2026 00:21Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amemuonya Rais wa Marekani Donald Trump dhidi ya kufanya maamuzi yanayotegemea taarifa zisizo sahihi, akisisitiza kuwa Iran haijawahi kutafuta, haitafuti, wala haitawahi kutafuta silaha za nyuklia.
-
Iran na Gambia zapania kuimarisha uhusiano wa pande mbili
Feb 25, 2026 05:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi na mwenzake wa Gambia wamesisitiza haja ya kusimamisha uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili katika nyanja zote zenye maslahi ya pande mbili.
-
Araghchi asisitizia fursa ya kufikia mwafaka na US, kulindwa mamlaka ya nchi kwa gharama yoyote
Feb 25, 2026 03:30Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema Iran na Marekani zina "fursa ya kihistoria" iliyopo mbele ya macho ya kufikia "makubaliano ambayo hayajawahi kushuhudiwa," huku akionya kwamba Jamhuri ya Kiislamu italinda uhuru na mamlaka yake ya kujitawala kwa gharama yoyote endapo kutakuwa na uvamizi mpya wa kijeshi wa Marekani.
-
Mohajerani: Iran inafadhilisha diplomasia badala ya vita
Feb 24, 2026 22:57Msemaji wa serikali ya Iran amesema, Jamhuri ya Kiislamu inafadhilisha diplomasia kuliko vita, lakini inaviona viwili hivyo kama mikakati ya kulinda maslahi ya taifa la Iran.
-
Jibu kali la Iran kwa hatua ya Umoja wa Ulaya dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 24, 2026 22:53Katika kujibu hatua haramu ya Umoja wa Ulaya dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeyataja majeshi ya majini na anga ya nchi zote wanachama wa umoja huo kuwa mashirika ya kigaidi.