-
Ayatullah Khatami: Njama za kuigawa Iran kupitia machafuko zimefeli
Jan 16, 2026 08:53Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa nchini Tehran amesema kuwa, njama za maadui za kuigawa Iran kupitia mamluki wao kuzusha vurugu na machafuko hapa nchini zimefeli na kugonga mwamba.
-
Araqchi: Iran iko macho na imejiandaa dhidi ya uingialiaji wowote wa kigeni
Jan 16, 2026 07:44Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na China wamesisitiza umuhimu wa kudumisha utulivu, kuheshimu uhuru wa nchi, na nafasi muhimu ya kidiplomasia katika kuzuia kuongezeka mizozo na mivutano.
-
Pakistan: Hatutaruhusu anga yetu itumiwe kwa ajili ya kuishambulia Iran
Jan 16, 2026 07:44Serikali ya Pakistan imetangaza kuwa, katu haitataruhusu anga yake itumiwe kwa ajili ya kuishambulia kijeshi Iran.
-
Iran: US, Israel ziliwapa silaha, fedha wafanya ghasia nchini
Jan 15, 2026 23:24Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema Marekani na Israel zilipanga na kufanikisha ghasia zilizoshuhudiwa hapa nchini hivi karibuni, zikielekeza silaha na pesa taslimu kuchochea vurugu na uvunjifu wa utulivu, ikiwa ni sehemu ya mpango mpana wa kuibua mgawanyiko na mifarakano katika taifa hili.
-
Kwa nini njama zote za Marekani dhidi ya Iran daima zinafeli?
Jan 15, 2026 22:40Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kwamba, watu wa Iran wataendelea kusimama imara kulinda na kutetea nchi yao, akisisitiza kuwa, njama yoyote ya Marekani dhidi ya Iran itashindwa tu kama zilivyoshindwa njama zao zote za huko nyuma.
-
Nini lengo la mchezo wa takwimu wa Trump kuhusu waliofariki katika ghasia za Iran?
Jan 15, 2026 07:04Ikiwa ni katika fremu ya uingiliaji wake katika masuala ya ndani ya Iran, Rais Donald Trump wa Marekani amezindua sarakasi mpya ya takwimu kuhusu Iran.
-
Araghchi amwandikia barua Katibu Mkuu wa UN kuhusiana na machafuko na jinai zilizofanywa na magaidi mamluki nchini Iran
Jan 15, 2026 06:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na jinai zilizofanywa na magaidi mamluki katika machafuko na uvurugaji wa amani uliofanywa hivi karibuni hapa nchini.
-
IRGC yaonya kuhusu majibu makali kwa makosa ya kimahesabu ya Marekani na Israel
Jan 15, 2026 04:17Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) amezionya Marekani, Israel na mamluki wao wenye mienendo ya Daesh kwamba kosa lolote la kimahesabu litakabiliwa na majibu makali na ya kuangamiza.
-
Shamkhani: Shambulio la makombora kwenye kambi ya Al-Udeid ni ukumbusho wa azma ya Iran la kujibu mapigo
Jan 15, 2026 03:32Mshauri mkuu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ameonya kwamba shambulio la makombora la Juni mwaka jana kwenye Kituo cha Anga cha jeshi la Marekani cha Al-Udeid huko Qatar linapaswa kuwa ukumbusho kwa Rais Donald Trump kuhusu azma na uwezo wa Iran wa kujibu kitendo chochote cha uchokozi.
-
Vinara wa mashambulizi ya kigaidi katika ghasia za Iran wakamatwa
Jan 14, 2026 23:10Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran imesema inaendelea kuwatambua na kuwakamata vinara wa mashambulizi ya kigaidi hivi karibuni jijini Tehran kwa ushirikiano madhubuti wa wananchi.