Iran yawasilisha majibu kwa pendekezo la Marekani la kukomesha uchokozi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i138288-iran_yawasilisha_majibu_kwa_pendekezo_la_marekani_la_kukomesha_uchokozi
Iran imewasilisha mpango kamili wa kukomesha vita vya uchokozi wa Marekani na Israel, ikisisitiza kulipwa fidia kamili kwa uharibifu wa vita na kuondolewa vikwazo vyote.
(last modified 2026-05-12T03:43:03+00:00 )
May 12, 2026 03:40 UTC
  • Iran yawasilisha majibu kwa pendekezo la Marekani
    Iran yawasilisha majibu kwa pendekezo la Marekani

Iran imewasilisha mpango kamili wa kukomesha vita vya uchokozi wa Marekani na Israel, ikisisitiza kulipwa fidia kamili kwa uharibifu wa vita na kuondolewa vikwazo vyote.

Ripoti zinasema kwamba mpango huo pia unasisitiza kuachiliwa mali za Iran zinazozuiliwa na kutambuliwa mamlaka ya Iran juu ya Mlango-Bahari wa Hormuz.

Majibu ya Iran kwa mapendekezo ya Marekani yametolewa kupitia wapatanishi wa Pakistani na kuwasilishwa kwa Washington siku ya Jumapili.

Muda mfupi baadaye, Trump aliandika kwenye jukwaa lake la Truth Social kwamba: “Nimesoma majibu kutoka kwa wanaoitwa ‘Wawakilishi’ wa Iran. Sikuyapenda, hayakubaliki kabisa!”

Chanzo kimoja kimeliambia Shirika la Habari la Tasnim kwamba jibu la Tehran "linasisitiza haki za msingi za taifa la Iran" na linapinga mpango wa awali wa Washington, ambao Tehran iliuona kama jaribio la kulazimisha kusalimu amri kwa matakwa mengi ya Trump.

"Hakuna mtu yeyote nchini Iran anayeandika mpango wa kumfurahisha Trump. Timu ya mazungumzo inaandika kwa ajili ya haki za taifa la Iran. Ikiwa Trump hafurahishwa na majibu hayo, ni bora zaidi," kimesema chanzo hicho na kusisitiza: "Trump hapendi ukweli; ndiyo maana anaendelea kushindwa dhidi ya Iran."

Mapema Jumapili Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, alikuwa amesisitiza kwamba mazungumzo hayana maana na kurudi nyuma na kulegeza kamba mbele ya matakwa ya Marekani.

"Kamwe hatutapiga magoti mbele ya adui, na ikiwa kuna mazungumzo au mjadala, haimaanishi kujisalimisha au kurudi nyuma," alisema Rais Pezeshkian kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X.

Shirika la Habari la Ian (IRNA) linasema jibu la Iran linasisitiza kwamba mazungumzo ya sasa kati ya Iran na Marekani yanapaswa kuzingatia juhudi za kukomesha vita, na masuala mengine, ikiwa ni pamoja na mizozo inayohusu mpango wa nyuklia wa Iran, yanapaswa kujadiliwa katika hatua za baadaye za mazungumzo.

Limesisitiza kwamba jibu la Iran linalenga juhudi za kukomesha uchokozi katika pande zote, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon, na kuhakikisha usalama wa usafirishajai wa meli katika Ghuba ya Uajemi.