Baqaei: Marekani inaendelea kusisitiza mawazo yaliyobuniwa na utawala wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i138290-baqaei_marekani_inaendelea_kusisitiza_mawazo_yaliyobuniwa_na_utawala_wa_israel
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Marekani inaendelea kung'ang'ania fikra na mawazo ya utawala wa Israel.
(last modified 2026-05-12T03:49:00+00:00 )
May 12, 2026 03:43 UTC
  • Esmail Baqaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
    Esmail Baqaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Marekani inaendelea kung'ang'ania fikra na mawazo ya utawala wa Israel.

Esmail Baqaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu mazungumzo kati ya Trump na Netanyahu na majibu yao kwa mpango wa Iran: Kitu pekee tulichodai ni haki halali za Iran. Je, takwa la Iran la kukomesha vita na kusimamishwa uharamia wa baharini dhidi ya meli za Iran, na takwa la kuachuliwa mali za watu wa Iran ambazo zimezuiwa bila haki kwa miaka mingi, ni kupita kiasi? Amehoji Baqaei na kusema: Je, pendekezo letu la upitaji salama katika Mlango-Bahari wa Hormuz ni ni takwa lililochupa mipaka? Na je, kurejeshwa usalama katika eneo la Magharibi mwa Asia na kaskazini mwa Lebanon ni kupita kiasi?

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, tumetoa mapendekezo mengi si kwa maslahi ya Iran tu bali pia kwa eneo zima la Asia Magharibi. "Masuala haya yote yalitakiwa kujadiliwa katika kifurushi kilichopendekezwa, lakini kwa bahati mbaya, upande wa Marekani unaendelea kung'anga'ania mawazo na fikra zilizobuniwa na utawala wa Israel.

Kuhusu ziara ya Donald Trump nchini China, Esmail Baqaei amesema: Ziara ya Trump nchini China ni suala la pande hizo mbili na linawahusu wao yenyewe. Amesema: China ni mmoja wa washirika wetu wa kimkakati ambao tunawasiliana nao mara kwa mara. "Wachina wanajua vyema misimamo yetu na wanajua kwamba vita vilivyonzishwa dhidi ya Iran si suala la kupita, bali ni sehemu ya mwelekeo wa kimataifa wa kuimarisha sera za kujichukulia maamuzii ya upande mmoja za Marekani", amesema Baqaei. Ameongeza kuwa, utulivu wa Asia Magharibi ni muhimu kwa China kama ulivyo muhimu kwetu na arafiki zetu wa China wanajua vizuri jinsi ya kutumia fursa hiyo.

Kuhusu madai ya Marekani dhidi ya Iran, Baqai amesema: Iran imethibitika kuwa nguvu inayowajibika katika eneo la Magharibi mwa Asia, na wakati huo huo, tunapinga uonevu. Amesema: Inatosha kuangalia utendaji wa Iran. Je, Iran ndiyo iliyoanzisha uvamizi? Je, tulifanya mauaji mara mbili wakati wa mazungumzo?