-
Kiongozi wa Mapinduzi asisitiza juu ya kuimarishwa utayari wa kivita wa jeshi la wanamaji.
Nov 29, 2023 08:14Akizungumza karibuni katika kikao na Kamanda Mkuu pamoja na makamanda wengine wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria uwezo mkubwa wa jeshi hilo hasa katika utekelezaji wa siasa za kiuchumi baharini na kusisitiza ulazima wa kuvumbuliwa uwezo mpya kwa ajili ya kuimarisha Mfumo na taifa na vilevile kuleta matumaini na uchangamfu katika jamii.
-
Marekani yauzuia ujumbe wa Iran kushiriki kikao cha Baraza la Usalama la UN
Nov 29, 2023 06:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza kuwa, ujumbe wa nchi hii umeshindwa kuhudhuria kikao cha leo cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa sababu Marekani imechelewa kutoa viza.
-
Iran yataka ICC iwafungulie mashitaka watawala watenda jinai Israel kuhusu uhalifu wa kivita Gaza
Nov 28, 2023 23:50Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian ameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuanzisha mahakama maalumu itakayowafungulia mashitaka watawala wa Israel kwa uhalifu wa kivita katika Ukanda wa Gaza, huku utawala huo ghasibu ukiendelea na kampeni yake ya mauaji ya kimbari katika eneo hilo lililozingirwa.
-
Iravani: Makombora ya Iran ya mipango ya anga za juu inafuata sheria za kimataifa
Nov 28, 2023 23:49Balozi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema mipango ya nchi hii ya makombora na anga ya juu inafuata sheria za kimataifa kikamilifu.
-
Kiongozi Mkuu: Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni rasilimali kubwa ya Mfumo na nchi
Nov 28, 2023 10:52Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya ulazima wa kutambuliwa uwezo na fursa mpya kwa ajili ya kuongeza nguvu na uwezo wa mfumo na nchi, pamoja na kujenga ukakamavu na matumaini katika jamii.
-
Iran yazionya Marekani na Israel juu ya 'matokeo hasi makali' endapo jinai za kivita zitaendelea Gaza
Nov 28, 2023 09:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amezionya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba zitakabiliwa na "matokeo hasi makali" iwapo zitashindwa kukomesha kikamilifu uhalifu wa kivita katika Ukanda wa Gaza uliofanywa wakati wa vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya eneo Palestina lililowekewa mzingiro.
-
Jeshi la Iran: Manowari ya Kimarekani yakubaliwa kuingia Ghuba ya Uajemi baada ya kujibu maswali yote ya Wanamaji wa Iran
Nov 28, 2023 04:14Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC amesema: Meli ya kubeba ndege za kivita ya Marekani ilikubaliwa kuingia Ghuba ya Uajemi kupitia Lango Bahari la Hormuz baada ya kujibu maswali yote ya vikosi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa lugha ya kifarsi.
-
Sisitizo la Naibu Waziri Mkuu wa Russia juu ya kuimarishwa uhusiano wa Moscow na Tehran
Nov 28, 2023 03:50Katika mazungumzo yake Jumtatu na Kazem Jalali, balozi wa Iran mjini Moscow, Alexander Novak Naibu Waziri Mkuu wa Russia amesisitiza juu ya kuimarishwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
-
Nchi za dunia zataka kununua manuwari za kivita za Iran
Nov 27, 2023 23:02Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, maendeleo ya jeshi la majini la Iran ni makubwa sana katika mikondo ya bahari kubwa duniani kiasi kwamba nchi mbalimbali zimeonesha hamu ya kununua manuari za Iran.
-
Baqeri: Manowari ya Deylaman kudhamini usalama kaskazini mwa Iran
Nov 27, 2023 08:57Mkuu wa Komandi Kuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kujiunga manowari mpya ya Deylaman kwenye orodha ya meli za kivita za Iran kutaimarisha usalama katika Bahari ya Caspian, kaskazini mwa nchi.