Nov 28, 2023 07:44 UTC
  • Jeshi la Iran: Manowari ya Kimarekani yakubaliwa kuingia Ghuba ya Uajemi baada ya kujibu maswali yote ya Wanamaji wa Iran

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC amesema: Meli ya kubeba ndege za kivita ya Marekani ilikubaliwa kuingia Ghuba ya Uajemi kupitia Lango Bahari la Hormuz baada ya kujibu maswali yote ya vikosi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa lugha ya kifarsi.

Kwa mujibu wa IRNA, Admeli Alireza Tangsiri, Kamanda wa Jeshi la Majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika mahojiano na vyombo vya habari Jumatatu usiku, alipongeza Siku ya Jeshi la Wanamaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kuongeza kuwa: 'Wamarekani wanapaswa kuwa na mienendo ya kimantiki katika Ghuba ya Uajemi, kwa sababu wanapoingia eneo hilo wanaweza kushambuliwa na Jeshi la Wanamaji la IRGC na Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.'

Akizungumzia kuingia manowari ya kubeba ndege za kivita ya Marekani katika Ghuba ya Uajemi katika siku chache zilizopita, Admeli Tangsiri amesema: 'Ndege zisizo na rubani za Iran zilikuwa juu yao na onyo lilitolewa kwamba helikopta za Marekani haziruhusiwi kupaa kutoka kwenye meli hiyo, na Wamarekani wakatii amri zote za jeshi za Iran.'

Meli ya Kimarekani katika Ghuba ya Uajemi

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: 'Harakati zote za majeshi ya kigeni katika Ghuba ya Uajemi zinafuatiliwa kwa karibu, na mara hii askari wa Marekani walipoingia katika eneo hilo, walifuata sheria na kuonyesha ushirikiano zaidi kuliko wakati uliopita.'

Sardar Tangsiri ametathmini uwepo wa meli za Marekani katika eneo kama njia pekee ya kuzitia moyo pande nyingine na wala si ishara ya nguvu na kusema: 'Siku ambayo Iran iliwakamata wanajeshi 10 wa Kimarekani maili tano kutoka kisiwa cha Iran, manowari 2 zilizobeba ndege za kivita 150 na meli nyingine tano za kivita za Marekani zilikuwa katika Ghuba ya Uajemi.

Tarehe 12 Januari 2016, Jeshi la Wanamaji la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu liliwatia mbaroni wanajeshi 10 wa Marekani ambao waliingia katika maji ya Iran kinyume cha sheria wakiwa na meli mbili za kijeshi, kilomita chache kutoka Kisiwa cha Farsi na kufungwa kwa siku kadhaa kisiwani humo.

 

Tags