-
Mfalme Salman bin Abdul-Aziz amwalika Rais wa Iran kutembelea Saudi Arabia
Mar 20, 2023 00:53Naibu Mkuu wa ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inayohusika na masuala ya kisiasa amesema kuwa, Mfalme wa Saudia Salman bin Abdul-Aziz amemtumia barua ya mwaliko Rais Ibrahim Raisi ili akaitembelee Saudi Arabia.
-
Amir-Abdollahian: Karibuni hivi nitakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia
Mar 19, 2023 10:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametangaza kuwa, atakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia mnamo siku chache zijazo na akasema: "tulikubaliana kuwa jumbe za kiufundi za pande zote mbili zitembelee balozi na balozi ndogo na kufanya maandalizi ya kivitendo ya kufunguliwa tena balozi hizo."
-
Iran yawahukumu adhabu ya kifo magaidi wa shambulizi la Shah cheragh
Mar 19, 2023 02:47Mahakama ya Iran imetoa hukumu ya kifo kwa watu wawili kwa kuhusika katika shambulio la kigaidi la Oktoba mwaka jana kwenye Harama ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), Shah Cheragh, katika mji wa kusini wa Shiraz.
-
Gharibabadi: Wairani 13,000 wameuawa kwa silaha za kemikali za nchi za Magharibi
Mar 18, 2023 10:39Afisa wa ngazi ya juu wa haki za binadamu wa Iran ameeleza kusikitishwa kwake na azimio la Bunge la Ulaya kuhusu tuhuma za kupewa sumu baadhi ya wanafunzi katika shule za Iran, akisisitiza kwamba maelfu ya Wairani walipoteza maisha kutokana na silaha za kemikali za nchi za Magharibi zilizotolewa kwa utawala wa Baath wa Iraq wakati wa utawala wa Saddam Hussein.
-
Kan'ani: Bunge la Ulaya limegeuka na kuwa jukwaa la chuki dhidi ya Iran
Mar 18, 2023 04:34Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekosoa shutuma "zisizo na msingi" zinazotolewa na wabunge wa Umoja wa Ulaya kuhusu kadhia ya kupewa sumu wanafunzi katika shule za Iran, ikisema bunge hilo sasa limegeuka kuwa jukwaa la chuki dhidi ya Iran.
-
Iran yalaani "unafiki' wa Ujerumani kuhusiana na silaha za nyuklia za Israel
Mar 18, 2023 00:38Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani msimamo wa Ujerumani akisema ni wa "kinafiki" kuhusu mpango wa amani wa nyuklia wa Iran huku nchi hiyo ya Ulaya ikinyamazia kimya silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni wa Israel ambazo ni "tishio kwa eneo na dunia nzima".
-
Iran yafungua kituo cha kisasa kabisa cha matibabu ya saratani Asia Magharibi
Mar 17, 2023 09:19Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ebrahim Raisi amezindua kituo cha kisasa kabisa cha matibabu ya saratani mjini Tehran na akasema serikali yake inalenga kuboresha maisha ya wananchi kuondoa udhaifu uliokuwepo.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Adui alikosea katika hesabu zake
Mar 17, 2023 09:18Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya wiki hii mjini Tehran amesisitiza kuwa: adui amefanya makosa katika hesabu zake huku taifa la Iran likichagua mantikiya Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Amir Abdollahian: Uhusiano kati ya Tehran na wakala wa IAEA uko kwenye njia sahihi
Mar 17, 2023 03:26Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema katika mazungumzo ya simu na Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, kwamba uhusiano kati ya Tehran na Wakala wa Kimataifa wa Nishatii ya Nyuklia uko kwenye mkondo sahihi.
-
Shamkhani: Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi uchukue nafasi ya mifarakano na uhasama
Mar 16, 2023 22:57Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesisitiza stratejia isiyobadilika ya sera za nje za Jamhuri ya Kiislamu kuhusu ushirikiano wa pande zote, endelevu na wenye manufaa na majirani zake na kusema: ili kuondokana na changamoto zilizopo ambazo kuendelea kwake hakuna maslahi kwa nchi yoyote katika eneo hili, ni lazima ushirikiano na mshikamano vichuke nafasi ya mifarakano na uhasama.