-
Bunduki 9,300 zimenaswa katika machafuko ya karibuni nchini Iran
Jan 23, 2023 07:43Msemaji wa Kamandi ya Polisi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa silaha 9,300 zimekamatwa wakati wa machafuko yaliyozuka hapa nchini hivi karibuni.
-
Abdollahian asisitiza azma ya Iran ya kuimarisha ushirikiano na bara la Afrika
Jan 23, 2023 03:50Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya azma ya Tehran ya kukuza na kustawisha zaidi ushirikiano wake na mataifa ya Kiafrika.
-
Iran itatoa jibu kwa hatua ya kuwekwa Jeshi la IRGC katika orodha ya 'kigaidi' EU
Jan 23, 2023 01:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameuonya Umoja wa Ulaya kuhusu hatua za "kujibu mapigo" baada ya Bunge la Ulaya kupiga kura ya kuongeza Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika orodha ya makundi ya 'kigaidi' ya Umoja wa Ulaya.
-
Iran yazindua awamu ya operesheni ya mradi wa Satalaiti wa Jenerali Soleimani
Jan 23, 2023 01:24Mkuu wa Shirika la Anga za Juu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuzinduliwa kwa awamu ya operesheni ya mradi wa kwanza wa mfumo wa satelaiti nchini, uliopewa jina la kamanda wa ngazi ya juu wa kupambana na ugaidi wa Iran, Jenerali Qassem Soleimani.
-
Raisi: Jeshi la IRGC limesitisha shari za magaidi katika eneo
Jan 22, 2023 08:06Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria hatua ya Bunge la Ulaya dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kueleza kuwa jeshi la IRGC limekabiliana na magaidi na kuzima shari za magaidi katika eneo la Asia Magharibi.
-
Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu yalaani vikali kitendo cha uchochezi dhidi ya IRGC
Jan 22, 2023 08:00Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu imetuma ujumbe na kulaani vikali hatua ya Bunge la Ulaya dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
-
Kiwewe cha nchi za Ulaya kwa nafasi ya kudhamini usalama ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Jan 22, 2023 04:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema katika mazungumzo ya simu aliyofanya na mwenzake wa Uswisi Tobias Billström kwamba, nchi za Ulaya zina deni la malipo ya shukrani kwa juhudi kubwa za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kupambana na ugaidi na akabainisha kwamba: Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) liliiokoa miji mikuu ya Ulaya na mashambulizi ya DAESH (ISIS).
-
Iran, Pakistan, Uturuki zalaani kuchomwa moto nakala ya Qurani Sweden
Jan 22, 2023 04:34Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imejiunga na ulimwengu wa Kiislamu katika kulaani vikali kitendo cha kuchomwa moto nakala ya Qur'ani Tukufu nchini Sweden.
-
Iran na Zimbabwe kusaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano
Jan 22, 2023 04:21Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Zimbabwe zinanatazamiwa kusaini hati kadhaa za makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili ndani ya wiki kadhaa zijazo.
-
Iran: Azimio la EU dhidi ya IRGC ni sehemu ya vita mseto dhidi ya taifa hili
Jan 22, 2023 00:08Wakuu wa mihimili mitatu ya serikali ya Iran sanjari na kulaani kitendo cha Bunge la Ulaya cha kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika orodha ya kile kinachodaiwa ni makundi ya kigaidi wamesitiza kuwa, hatua hiyo ni sehemu ya vita vya mseto dhidi ya taifa hili.