Iran yazindua awamu ya operesheni ya mradi wa Satalaiti wa Jenerali Soleimani
Mkuu wa Shirika la Anga za Juu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuzinduliwa kwa awamu ya operesheni ya mradi wa kwanza wa mfumo wa satelaiti nchini, uliopewa jina la kamanda wa ngazi ya juu wa kupambana na ugaidi wa Iran, Jenerali Qassem Soleimani.
Hassan Salarieh alitoa tangazo hilo kwenye tovuti rasmi ya Shirika hilo siku ya Jumapili alipokuwa akifafanua kuhusu hali ya hivi punde ya utekelezaji wa mradi wa satalaiti wa Jenerali Soleimani, ambao ni sehemu ya mpango unaoendelea wa miaka 10 wa anga za juu wa Iran.
Salarieh amesema, "Kulingana na mpango wa anga za juu wa miaka 10 na ili kutoa huduma kwa wananchi, taasisi za serikali na mashirika na pia kutoa huduma kwa makampuni ya sekta binafsi, Shirika la Anga la Iran limepewa jukumu la kuweka mfumo wa satelaiti ya mawasiliano katika mzingo wa sayari ya dunia."
Aidha amesema: "Utekelezaji wa mradi huo, unaoitwa "Mradi wa Shahidi Soleimani' na unachukuliwa kuwa mradi wa kwanza wa mfumo wa satelaiti katika nchi yetu, ni muhimu sana kutokana na mafanikio katika utengenezaji wa satelaiti."
Salarieh amebaini kuwa katika muda wa chini ya mwezi mmoja tangu kuidhinishwa kwa programu ya anga ya juu ya miaka 10, mojawapo ya vifungu muhimu zaidi ni utekelezaji wa Mradi wa Shahidi Soleimani.
Akisifu hatua zilizochukuliwa na Shirika hilo katika uga wa kuunda satelaiti ndogo, Salarieh alisema, "Inasikitisha kwamba baada ya mafanikio katika hatua hii, njia ya kukamilisha na kuendeleza mifumo ya satelaiti na kutoa huduma zaidi itaandaliwa katika hatua zinazofuata."
Iran ilirusha satelaiti yake ya kwanza ya Omid (Matumaini) mnamo 2009 na satelaiti yake ya Rasad (Ufuatiliaji) ilitumwa kwenye oanga za mbali mnamo 2011. Mnamo mwaka wa 2012, Jamhuri ya Kiislamu ilifanikiwa kuweka satelaiti yake ya tatu iliyotengenezwa nchini, Navid (Habari Njema), kwenye anga za mbali
Mnamo Aprili 2020, Iran ilitangaza kurusha kwa mafanikio satelaiti yake ya kwanza ya kijeshi kwenye obiti. Na mnamo Machi 2022, Iran ilirusha satelaiti yake ya pili ya kijeshi katika anga za ambali. Mafanikio hayo ya Iran yameweza kufikiwa pamoja na kuwa nchi hii imewekewa vikwazo na madola ya Magharibi yakiongoziwa na Marekani.