Abdollahian asisitiza azma ya Iran ya kuimarisha ushirikiano na bara la Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i93210-abdollahian_asisitiza_azma_ya_iran_ya_kuimarisha_ushirikiano_na_bara_la_afrika
Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya azma ya Tehran ya kukuza na kustawisha zaidi ushirikiano wake na mataifa ya Kiafrika.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Jan 23, 2023 03:50 UTC
  • Abdollahian asisitiza azma ya Iran ya kuimarisha ushirikiano na bara la Afrika

Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya azma ya Tehran ya kukuza na kustawisha zaidi ushirikiano wake na mataifa ya Kiafrika.

Hussein Amir-Abdollahian amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo kwa nyaraka tofauti hapa mjini Tehran na wakuu wa timu na jumbe saba za Kiafrika zilizoko hapa mjini Tehran.

Baadhi ya wakuu wa jumbe hizo waliokuja hapa Tehran kwa ajili ya kushiriki katika kongamano la kwanza la kimataifa la wanawake wenye taathira ni kutoka mataifa ya Senegal, Nigeria, Burkina Faso, Guinea Conakry, Cameroon na Guinea Bissau.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  amesisitiza katika mazungumzo hayo kwamba, Tehran ina azma thabiti ya kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Afrika katika nyanja mbalimbali hususan katika uga wa kiuchumi.

Wakati huo huo, wakuu wa jumbe zilizoshiriki kongamano la kwanza la wanawake wenye taathira sambamba na kusisitiza juu ya udharura wa kudumishwa makongamano kama haya wamesifu nafasi muhimu ya wanawake wa Kiirani katika jamii.

Kongamano la kwanza la kimataifa la wanawake wenye taathira lilifanyika hapa mjini Tehran Ijumaa iliyopita na kuhudhuriwa na wanawake kutoka nchi 96 duniani katika mabara matano duniani wakiwemo wake za marais wa zamani wa Niger, Sri Lanka, Guinea na mke wa Waziri Mkuu wa Armenia,