Baqaei: Kukabiliana na ugaidi ni jukumu la kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i138030-baqaei_kukabiliana_na_ugaidi_ni_jukumu_la_kimataifa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Mali.
(last modified 2026-04-28T10:31:30+00:00 )
Apr 28, 2026 09:41 UTC
  • Esmail Baqaei
    Esmail Baqaei

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Mali.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran (IRNA), Esmail Baqaei msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea katika maeneo tofauti ya Mali ambayo yamepelekea kuuawa “Sadio Camara,” waziri wa ulinzi, watu wa familia yake, na idadi kubwa ya wananchi wa nchi hiyo. 

Baqaei, ametoa rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na kueleza mshikamano wa Iran na serikali na watu wa Mali. Vilevile amewaombea ahueni na pona ya haraka majeruhi wa mashambulizi hayo. 

Akisisitiza misimamo ya kimsingi ya Iran katika kulaani kwa dhati aina zote za ugaidi na misimamo mikali ya ukatili, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa kukabiliana na ugaidi ni jukumu la kimataifa linalohitaji ushirikiano na uratibu wa mataifa yote, na mapambano endelevu dhidi ya watenda uhalifu, waandaaji, waungaji mkono na wafadhili wa ugaidi. 

Baqaei ameeleza matumaini yake kwamba taifa la Mali, kwa umoja na mshikamano, litashinda ugaidi na wanaungaji mkono na wafadhili wake.