-
Admeri Irani awaonya Wamarekani: Manowari ya Lincoln ikija karibu, tutalipiza kisasi cha damu ya mashahidi wa Dena.
Mar 30, 2026 01:54Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaonya Wamarekani akisema: "Mara tu manowari ya kubeba ndege ya Abraham Lincoln itakapokaribia eneo letu la ulengaji shabaha, tutalipiza kisasi cha damu ya mashahidi wa manowari ya Dena kwa kurusha aina mbalimbali ya makombora kutoka pwani hadi baharini."
-
Jeshi la Iran: Wanajeshi wa Marekani watageuzwa kuwa “Chakula cha Papa”
Mar 29, 2026 23:17Msemaji wa Kamandi ya Khatam al‑Anbia ya Jeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonya kuwa uvamizi wowote wa kijeshi wa Marekani kupitia nchi kavu au jaribio la kuikalia kwa mabavu ardhi ya Iran utamalizika kwa madhara makubwa, akisema askari wa Marekani watakumbana na maangamizi na hata kugeuka “chakula cha papa” katika Ghuba ya Uajemi.
-
Spika wa Bunge: Iran imekataa matakwa ya Marekani na Israel ya “Kujisalimisha,” Itapigana hadi ushindi
Mar 29, 2026 23:09Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema Iran haitakubali kamwe masharti ya kujisalimisha yanayotolewa na Marekani na Israel, na itaendelea kupigana hadi ipate ushindi.
-
Kwa nini jiografia inaipa Iran nafasi nzuri katika Lango-Bahari la Hormuz?
Mar 29, 2026 08:56Lango Bahari la Hormuz takriban limefungwa kwa wiki nne sasa na hivyo kupelekea soko la mafuta duniani kutumbukia katika mgogoro mkubwa wa nishati na wala haijulikani litafunguliwa lini.
-
Iran yaangusha ndege nyingine ya kivita aina ya F 16 ya adui
Mar 29, 2026 00:02Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetangaza kwamba wimbi la 85 la Operesheni Ahadi ya Kweli 4 lilitekelezwa, kwa kushambulia viwanda kadhaa vikubwa vya adui na kuharibu ndege nyingine ya kivita ya F-16 ya adui.
-
Qalibaf: Jibu la Iran limepangwa ili kuharakisha kusambaratika jeshi la Israel
Mar 29, 2026 05:57Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amezungumzia kukiri kamanda wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kusambaratika jeshi hilo na kuandika: Jibu la Iran limeratibiwa kwa namna ambayo linaharakisha kusambaratika jeshi la Israel.
-
Baqaei: Mashambulizi dhidi ya vyuo vikuu yanaonyesha chuki ya adui kwa maendeleo ya kisayansi ya Wairani
Mar 29, 2026 05:26Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali jinai za adui za kuvishambulia vyuo viku na vituo vya elimu nchini Iran.
-
Mashambulizi ya Iran yaua au kujeruhi zaidi ya wanajeshi 500 wa Marekani waliokuwa wamejificha UAE
Mar 29, 2026 03:23Jeshi la Iran lilitangaza siku ya Jumamosi kuwa vikosi vyake vimeua au kuwajeruhi zaidi ya wanajeshi 500 wa Marekani katika mashambulizi yaliyolenga maficho mawili ya Marekani huko Dubai.
-
Iran yatafakari kujiondoa mkataba wa nyuklia wa NPT
Mar 29, 2026 01:06Ripoti zinaonyesha kuwa suala la kujiondoa katika Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT) sasa limewekwa katika ajenda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Rais wa Iran, aonya kuwa Israel inalenga kueneza vita katika kanda ya Asia Magharibi
Mar 29, 2026 01:05Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ameonya katika mazungumzo yake ya simu na Waziri Mkuu wa Pakistan, kuhusu malengo hatari ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kupanua vita hadi nchi nyingine za kanda ya Asia Magharibi.