Iran yaangusha ndege nyingine ya kivita aina ya F 16 ya adui
Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetangaza kwamba wimbi la 85 la Operesheni Ahadi ya Kweli 4 lilitekelezwa, kwa kushambulia viwanda kadhaa vikubwa vya adui na kuharibu ndege nyingine ya kivita ya F-16 ya adui.
IRGC imesema operesheni hiyo lilitekelezwa kwa jina la msimbo la “Ya Rasulullah” na kwa ajili ya kuwaenzi raia na watumishi waliouawa shahidi hivi karibuni walipokuwa wakitumikia sekta ya viwanda hapa nchini.
Taarifa hiyo imesema: “Baadhi ya viwanda vikubwa vinavyomilikiwa na adui Mmarekani‑Mzayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na maeneo mengine vimepigwa kwa makombora na ndege zisizo na rubani, na sehemu zake zimeharibiwa.”
Taarifa hiyo imesema kuwa: “Wakati wa operesheni hiyo kubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani, jeshi la anga la adui lilijaribu kulenga vizindua-makombora vyetu kwa kutuma ndege za kivita na droni, lakini ulinzi wa anga wa IRGC ulidungua ndege ya kimkakati isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ‑9 katika anga ya Shiraz, na ndege ya kivita ya Marekani aina ya F‑16 ilipigwa kusini mwa mkoa wa Fars na kuanguka kabla ya kutua katika uwanja wa ndege nchini Saudi Arabia. Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) imethibitisha kuwa ndege hiyo ilipigwa na kuharibika kabisa.”
Taarifa ya IRGC imehitimisha kwa kusema: “Tumekwishawaonya watawala wasio na hekima wa Marekani kwamba tutalipiza kisasi kwa mashambulizi dhidi ya viwanda vyetu. Shambulizi hili lilikuwa onyo tu; iwapo mashambulizi dhidi ya sekta ya viwanda yatafanyika tena, majibu yajayo yatakuwa zaidi ya matarajio yenu.”
Juzi pia Ndege ya kivita aina ya F-18 ya jeshi la kigaidi la Marekani ilipigwa na kutunguliwa kwa kombora la Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kusini mwa nchi.
Ndege kadhaa za kivita za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zimetunguliwa kwa kutumia makombora ya Iran wakati zikiwa zinatakeleza operesheni za kivita. Aidha Idadi ya ndege zisizo na rubani za maadui zilizotunguliwa na ulinzi wa anga wa Iran hadi sasa inafikia karibu ndege 140.