Qalibaf: Jibu la Iran limepangwa ili kuharakisha kusambaratika jeshi la Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137664-qalibaf_jibu_la_iran_limepangwa_ili_kuharakisha_kusambaratika_jeshi_la_israel
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amezungumzia kukiri kamanda wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kusambaratika jeshi hilo na kuandika: Jibu la Iran limeratibiwa kwa namna ambayo linaharakisha kusambaratika jeshi la Israel.
(last modified 2026-03-29T05:57:50+00:00 )
Mar 29, 2026 05:57 UTC
  • Muhammad Baqir Qalibaf
    Muhammad Baqir Qalibaf

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amezungumzia kukiri kamanda wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kusambaratika jeshi hilo na kuandika: Jibu la Iran limeratibiwa kwa namna ambayo linaharakisha kusambaratika jeshi la Israel.

Muhammad Baqir Qalibaf ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba: Kamanda wa jeshi la Israel amesema katika mkutano wa baraza la mawaziri: "Ninainua bendera kumi nyekundu... jeshi la Israel litajiangusha lenyewe".

Qalibaf ameeleza kuwa utawala wa Israel, kwa kuzidisha mvutano na kushambulia miundombinu ya viwanda ya Iran, unataka kupuuza tahadhari hizi na kurejesha hali ya kujiamini kwa baraza lake la mawaziri na jeshi hilo lililoshindwa kwa jinai chungu nzima.

Amesema kuwa jibu la Iran limepangwa ili kuharakisha kusambaratika huko kunakoendelea ndani ya jeshi la Israel.