-
Kuanza urutubishaji wa urani wa asilimia 60 katika kituo cha Fordo; radiamali ya Iran kwa hatua za uhasama za Magharibi
Nov 24, 2022 03:47Ikiwa ni katika kujibu azimio la hivi karibuni la Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran limetangaza uzalishaji wa urani iliyorutubishwa hadi kiwango cha asilimia 60 katika kituo cha Fordo.
-
Raisi: Machafuko ni kigingi kwa mazungumzo na ustawi wowote
Nov 23, 2022 23:02Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria namna serikali ilivyo na sikio la kusikia malalamiko na maoni ya upinzani na kueleza kuwa: machafuko yanazuia mazungumzo na kupatikana ustawi wa aina yoyote.
-
Kukiri Grossi kuhusu kutokuwepo mpango wa kijeshi wa nyuklia nchini Iran
Nov 23, 2022 22:52Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA akijibu swali kuhusu uwezekano wa Iran kupata bomu la nyuklia amesema: "Katika kiwango cha sasa cha uzalishaji urani iliyorutubishwa, Iran imeweza kuzalisha kiwango cha kutosha cha kuiwezesha kutengeneza zaidi ya kifaa kimoja (cha mlipuko) iwapo itataka kufanya hivyo."
-
Iran: Madai ya Marekani na nchi za Magharibi kuhusu haki za binadamu hayana msingi wowote
Nov 23, 2022 08:39Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, madai ya haki za binadamu yanayotolewa na Maraekani, nchi za Magharibi ya vibaraka wao ni chapwa na hayana msingi wowote.
-
Jeshi la Sepah lawataka wakazi wa kaskazini mwa Iraq kuwa mbali na vituo vya magaidi
Nov 23, 2022 05:51Kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwamba jeshi hilo litaendeleza operesheni za nchi kavu dhidi ya makundi ya kigaidi yanayotaka kujitenga yaliyoko katika eneo la Kurdistan nchini Iraq hadi tishio hilo litakapotokomezwa na kupokonywa silaha magaidi hao.
-
Azma ya Iran ya kukabiliana na magaidi wanaotaka kujitenga kaskazini mwa Iraq
Nov 23, 2022 02:34Vikosi vya makombora na ndege zisizo na rubani za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mara nyingine tena vimelenga makao makuu ya makundi ya kigaidi ya Komoleh na Democratic katika mikoa ya Sulaymaniyah na Erbil nchini Iraq.
-
Iran yaanza urutubishaji urani katika kiwango cha asilimia 60
Nov 22, 2022 23:12Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran amesema: "Uzalishaji urani katika kiwango cha asilimia 60 umeanza katika Kituo cha Nyuklia cha Fordo."
-
Al Mayadeen: Silaha nyingi zilizotumiwa kwenye machafuko Iran zimeingizwa kupitia Kurdistan ya Iraq
Nov 22, 2022 08:10Televisheni ya Al Mayadeen imeeleza katika ripoti maalumu kuwa, silaha nyingi zilizoingizwa kimagendo nchini Iran kwa ajili ya kutumiika katika vitendo vya kigaidi, kuzusha machafuko na kuvuruga amani zimepitishwa kwa kutumia mpaka wa eneo la Kurdistan ya Iraq.
-
Rais Raisi: Kushika nafasi ya kwanza katika kanda kwenye sekta ya afya ni kielelezo cha ustawi wa Iran
Nov 21, 2022 12:14Rais Ebrahim Raisi amesema kushika nafasi ya kwanza katika eneo na ya kumi na tano duniani katika uga wa afya na tiba ni ishara na kielelezo cha maendeleo na ustawi wa nchi.
-
Iran yaamua kujibu kivitendo vikwazo vipya vya Ulaya na Marekani
Nov 21, 2022 03:49Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Tehran katika hatua ya awali imeazimia kujibu kwa njia tofauti, vikwazo vya hivi karibuni vya nchi tatu za Ulaya pamoja na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Itatoa majibu hayo kupitia taasisi yake ya nishati ya atomiki.