-
Mapinduzi ya Kiislamu na kusambaratika satwa ya madola ya kiistikbari duniani
Feb 11, 2022 11:30Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran tarehe 11 Februari 1979 ulikuwa tukio muhimu na la kipekee katika historia ya maelfu ya miaka ya Iran. Haya ni mapinduzi ambayo yalipelekea kuibuka mabadiliko ya kimsingi katika jamii ya Iran katika nyanja za kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
-
Ebrahim Raisi: Iran bado imeshikamana na nara ya "Si Mashariki si Magharibi"
Feb 11, 2022 07:09Rais Ebrahim Raisi amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran bado imeshikamana na nara yake ya "Si Mashariki, si Magharibi" ya tangu mwaka 1979.
-
"Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni jinamizi la mabeberu na kimbilio la wanyonge"
Feb 11, 2022 07:09Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu yameleta matumaini kwa wanyonge na wapigania ukombozi wa mataifa yao kama ambavyo yametia nguvu masuala ya kiroho na kimaanawi ulimwenguni.
-
Reuters: Usafirishaji mafuta ya Iran nje ya nchi umepindukia mapipa milioni 1 kwa siku
Feb 11, 2022 04:00Shirika la Habari la Reuters limetangaza kuwa, usafirishaji wa mafuta ghafi ya Iran nje ya nchi umepindukia mapipa milioni 1 kwa siku ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
-
Wairan leo wanaadhimisha miaka 43 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 10, 2022 23:27Leo Ijumaa tarehe 22 Bahman, sawa na tarehe 11 Februari, wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanaadhimisha sherehe za miaka 43 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini.
-
Iran: Kumalizika mazungumzo ya Vienna kunategemea kuondolewa vikwazo Tehran
Feb 10, 2022 23:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema muda wa kumalizika mazungumzo ya Vienna ya kujaribu kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA unategemea irada ya Wamagharibi ambao ni upande wa pili wa mazungumzo hayo, kuiondolewa vikwazo haramu Tehran.
-
Rais: Taifa la Iran limesimama kidete katika misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 10, 2022 08:38Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao na mabalozi wa nchi za nje hapa mjini Tehran kwa mnasaba wa kukumbuka ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: "Taifa la Iran limesimama imara katika misingi ya itikadi za mapinduzi yake."
-
Kamandi Kuu ya Vikosi vya ulinzi vya Iran: Hatua za kila upande zitachukuliwa kukabiliana na hujuma za maadui
Feb 10, 2022 04:50Kamandi Kuu ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza kuwa vikosi hivyo vitachukua hatua za kila upande dhidi ya hujuma mchanganyiko za maadui.
-
Raisi: Kuendelezwa sera zilizofeli za Trump ndiyo sababu hasa ya kutopiga hatua mazungumzo ya Vienna
Feb 10, 2022 00:07Rais Ebrahim Raisi amesema, kuendelezwa sera zilizofeli za serikali iliyopita ya Marekani ndicho kizuizi kikuu kinachokwamisha kupiga hatua za kuridhisha mazungumzo ya Vienna.
-
Iran yazindua kombora jipya la masafa ya mbali, lenye shabaha kali la Khaibar Shekan
Feb 09, 2022 10:06Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limezindua kombora jipya la masafa ya mbali na lenye shabaha kali la Khaibar Shekan.