-
Iran: Lengo la mazungumzo ya Vienna ni kuondolewa vikwazo vyote
Dec 06, 2021 03:42Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, lengo kuu la mazungumzo ya Vienna baina ya Iran na kundi la 4+1 na kuondolewa vikwazo vyote vya kidhulma ilivyowekewa Tehran.
-
Ebrahim Raisi: Tunafuatilia kwa nguvu kuondolewa vikwazo vyote
Dec 05, 2021 23:50Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema usiku wa kuamkia leo Jumatatu kwamba, Tehran inafuatilia kwa nguvu suala la kuondolewa vikwazo vyote vya kidhulma ilivyowekewa.
-
Araqchi: Marekani inabeba dhima kwa hali ya sasa Afghanistan
Dec 05, 2021 23:46Katibu wa Baraza la Kistratajia la Mahusiano ya Kigeni la Iran amesema Marekani ndiyo inayopaswa kulaumiwa na kuwabishwa kutokana na matatizo mengi yanaoikumba Afghanistan.
-
Iran: Hatutalegeza kamba katika kushinikiza kuondolewa vikwazo haramu
Dec 05, 2021 11:24Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya kisiasa amesema Jamhuri ya Kiislamu katu haitolegeza kamba katika mazungumzo ya Vienna, Austria na itaendelea kushinikiza kuondolewa vikwazo vya kidhalimu na vilivyo kinyume cha sheria vya Marekani dhidi ya taifa hili.
-
Ayatullah Khatami: Taifa la Iran halitokubali chochote ghairi ya kuondolewa vikwazo vyote
Dec 03, 2021 08:22Khatibu wa Muda wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesisitiza kuwa, taifa la Iran halitokubaliana na chochote katika mazungumzo yanayoendelea mjini Vienna Austria ghairi ya kuondolewa vikwazo vyote vya kidhulma lilivyowekewa taifa hili la Kiislamu na madola ya kibeberu.
-
Kamanda wa IRGC: Marekani iondoke karibu na ardhi ya Iran
Dec 03, 2021 01:17Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ameitaka Marekani iviondoe vikosi vyake katika maeneo yanayopakana na Jamhuri ya Kiislamu, kabla hawajafikiwa na hatima kama waliyopata huko Afghanistan.
-
Bagheri: Iran imewasilisha matini ya pendekezo lake kwa kundi la 4+1
Dec 02, 2021 08:49Mkuu wa Timu ya Iran katika Mazungumzo ya Kuondoa Vikwazo vya Kidhalimu dhidi ya Iran na ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayeshughulikia masuala ya kisiasa amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imewaslisha matini ya pendekezo lake kwa kundi la 4+1.
-
Kiongozi: Wanaojidai watetezi wa haki za binadamu duniani walitoa msukumo kwa jinai za Saddam
Dec 02, 2021 04:23Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria jinai zilizofanywa na dikteta wa Iraq Saddam dhidi ya watu wa Iran na akasema: Saddam alikuwa akifanya jinai hizo kwa msukumo na uungaji mkono wa wanaojigamba kuwa watetezi wa haki za binadamu duniani.
-
Austria: Tunafanya juhudi ili kufikiwe makubaliano ya nyuklia na Iran
Dec 01, 2021 23:31Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Austria imesema katika taarifa yake kuwa, nchi hiyo ambayo ni mwenyeji wa duru nyingine ya mazungumzo ya nyuklia inaunga mkono juhudi za pande zote katika mazungumzo hayo ili kuhakikisha kunafikiwa makubaliano.
-
Wamagharibi walivyohusika katika shambulio la silaha za kemikali lililofanywa Sardasht na utawala wa Saddam
Dec 01, 2021 23:28Jumuiya ya kutetea waathirika wa ugaidi imesema, Sardasht ni nembo ya haki za binadamu duniani na imesisitiza kuwa: lazima watu wote, taasisi na serikali zilizoshirikiana na utawala wa Saddam katika kutenda jinai kubwa zaidi ya utumiaji wa silaha za kemikali dhidi ya binadamu wakemewe na kusailiwa.