-
Rais Ibrahim Raeisi: Serikali ya Afghanistani inapaswa kuwa jumuishi
Sep 18, 2021 06:49Rais Ibrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kusisitiza kuwa, serikali itakayoundwa nchini Afghanistan inapaswa kuwa jumuishi amesema, serikali ya kaumu au mrengo fulani tu wa kisiasa haiwezi kuyapatia ufumbuzi matatizo.
-
Khatibzadeh: Uanachama wa Iran katika Jumuiya ya Shanghai ni wenzo muhimu wa siasa za nje kuhusu Asia
Sep 18, 2021 03:43Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa uanachama kamili wa Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ni hatua kubwa kuelekea uhusuano bora zaidi na ni wenzo muhimu wa siasa za nje za Tehran kuhusu eneo la Asia.
-
Iran: Tehran itaimarisha udiplomasia athirifu katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai
Sep 17, 2021 22:38Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran imezishukuru nchi wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwa kuikubali Jamhuri ya Kiislamu kama mwanachama kamili katika jumuiya hiyo na kusema kuwa: Tehran itatumia demokrasia athirifu kwa ajili ya kuimarisha mahusiano na nchi wanachama.
-
Rais Ibrahim Raeisi: Jumuiya ya Shanghai inaweza kuwa kichocheo cha mtazamo mmoja wa pande kadhaa
Sep 17, 2021 06:59Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) inaweza kuwa kichocheo muhimu cha mtazamo mmoja wa pande kadhaa ulimwenguni.
-
Russia yataka Iran iondolewe vikwazo vyote vya nyuklia ilivyowekewa
Sep 17, 2021 06:51Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika asasi za kimataifa zenye makao yake mjini Vienna Austria ametoa wito wa kuondolewa vikwazo vyote vya nyuklia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
GCC yarudia tena madai yake ya kila mara na ya kuchekesha dhidi ya Iran
Sep 17, 2021 03:43Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi GCC limetoa taarifa mwishoni mwa kikao chake kilichofanyika jana katika ngazi ya mawaziri wa mambo ya nje kwa kurudia tena madai ya huko nyuma dhidi ya Iran sambamba na kuomba tena nchi wanachama wa baraza hilo zishirikishwe kwenye mchakato wa mazungumzo ya nyuklia na Iran.
-
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran atahutubia mkutano wa mwaka huu wa Baraza Kuu la UN
Sep 16, 2021 22:49Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, Rais Ebrahim Raisi atahutubia mkutano wa mwaka huu wa Baraza Kuu la umoja huo katika siku ya kwanza ya mkutano huo.
-
Rais Ebrahim Rais afanya mazungumzo na viongozi wa Pakistan, Uzbekistan na Belarus
Sep 16, 2021 10:47Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasili katika mji mkuu wa Tajikistan, Dushanbe, ambako anashiriki mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai unaofanyika nchini humo leo na kesho.
-
Safari ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tajikistan; umuhimu na malengo yake
Sep 16, 2021 04:31Sayyid Ibrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Alkhamisi ya leo ameelekea Dushanbe, mji mkuu wa Tajikistan kwa ajili ya kushiriki na kuhutubia mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai unaofanyika nchini humo leo na kesho.
-
Baada ya wiki moja, Iran itakuwa imeshapiga chanjo ya corona, watu milioni 50
Sep 15, 2021 02:47Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran amesema kuwa, katika kipindi cha wiki moja ijayo, Jamhuri ya Kiislamu itakuwa imeshapiga chanjo ya corona watu milioni 50 humu nchini.