Rais Ibrahim Raeisi: Serikali ya Afghanistani inapaswa kuwa jumuishi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i74802-rais_ibrahim_raeisi_serikali_ya_afghanistani_inapaswa_kuwa_jumuishi
Rais Ibrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kusisitiza kuwa, serikali itakayoundwa nchini Afghanistan inapaswa kuwa jumuishi amesema, serikali ya kaumu au mrengo fulani tu wa kisiasa haiwezi kuyapatia ufumbuzi matatizo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 18, 2021 06:49 UTC
  • Rais  Ibrahim Raeisi: Serikali ya Afghanistani inapaswa kuwa jumuishi

Rais Ibrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kusisitiza kuwa, serikali itakayoundwa nchini Afghanistan inapaswa kuwa jumuishi amesema, serikali ya kaumu au mrengo fulani tu wa kisiasa haiwezi kuyapatia ufumbuzi matatizo.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo leo mjini Dushanbe Tajikistan katika mkutano wake wa pamoja na waandishi wa habari na Rais wa nchi hiyo Emomali Rahmon na kusisitiza udharura wa kupanuliwa ushirikiano wa kieneo.

Ibrahim Raeisi amesema, kwa bahati njema mitazamo yetu na Tajikistan kuhusiana na Afghanistan inakaribiana na mataifa haya mawili yanaamini kwamba, uingiliaji wa kigeni katika masuala ya ndani ya nchi hiyo umelisababishia taifa hilo mabalaa mengi na hivyo kuna haja ya kukata mikono ya maajinabi.

Rais wa Iran akihutubia katika mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai

 

Rais wa Iran sanjari na kusisitiza kwamba, uwepo wa magaidi nchini Afghanistan siyo tu kwamba, ni hatari kwa nchi hiyo bali ni tishio pia kwa eneo zima amesema kuwa, hii leo wamarekani ambao waliunda na kuasisi kundi la kigaidi la Daesh baada ya kundi hilo kufanya unyama huko Syria na Iraq walichukua hatua ya kulipeleka Afghanistan.

Kwa upande wake Rais Emomali Rahmon wa Tajikistan amesema katika mkutano huo na waandishi wa habari akiwa na Rais Raeisi kwamba, Iran ni rafiki wa Tajikistan ambapo sambamba na kuashiria mambo mengi ya pamoja zinayoshirikiana nchi mbili hizi kama utamaduni na dini, amesiisitiza juu ya udharura wa kupanuliwa zaidi uhusiano baina ya pande mbili.