-
Jenerali Salami: Vita vijavyo vitaashiria mwisho wa uhai wa Israel
Aug 08, 2021 03:29Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameukumbusha utawala wa Kizayuni juu ya uwezo mkubwa wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon katika mapambano na vita vya nchi kavu na kuonya kuwa, hatua yoyote ghalati itakayopelekea kuibuka vita vipya, haitakuwa na matokeo mengine isipokuwa kufutwa Israel katika uso wa dunia.
-
Iran: Mauaji ya Hiroshima ni kumbukumbu ya jinai za US dhidi ya binadamu
Aug 08, 2021 03:16Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema mashambulizi ya mabomu ya atomiki yaliyofanywa na Kikosi cha Anga cha Jeshi la Marekani dhidi ya miji ya Hiroshima na Nagasaki nchini Japan katika Vita Vya Pili Vya Dunia ndiyo jinai kubwa zaidi dhidi ya binadamu iliyowahi kuhuhudiwa katika uso wa dunia.
-
Iran yataka wahusika katika vita Afghansitan wasitishe mapingano
Aug 07, 2021 23:15Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa wito kwa pande zote katika vita nchini Afganistan kusitisha vita na mauaji ya ndugu kwa ndugu sambamba na kufanya mazungumzo ya kutatua mgogoro uliopo huku ikitangaza kuwa tayari kuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo.
-
Iran yakanusha madai yasiyo na msingi ya G7 kuhusu hujuma dhidi ya meli
Aug 07, 2021 23:11Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani taarifa isiyo na msingi ya nchi za kundi la G7 ambalo limeituhumu Tehran kuwa eti ilihusika na hujuma ya wiki iliyopita dhidi ya meli ya Israel katika pwani ya Oman.
-
Rais Ebrahim Raisi: Daima Iran itaendelea kutetea haki za wananchi wa Palestina
Aug 07, 2021 07:37Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, daima taifa hili litaendelea kuunga mkono na kutetea haki za wananchi wa palestina mkabala na uadui wa utawala vamizi wa Israel.
-
Balozi wa Iran UN: Baraza la Usalama lichukue hatua dhidi ya chokochoko za Israel katika eneo
Aug 07, 2021 03:34Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa Baraza la Usalama la umoja huo inapasa lichukue hatua ya kukabiliana na chokochoko zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo.
-
Qalibaf: Vita vya 'Upanga wa Quds' viliwapa izza Waislamu
Aug 06, 2021 20:37Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema vita vya siku 12 vya 'Upanga wa Quds' huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu viliwapa izza na kuwapandisha hadhi Waislamu kote duniani.
-
Raisi: Kuna fursa nzuri za kuimarisha uhusiano wa Iran na Tanzania, Zanzibar
Aug 06, 2021 10:28Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuna fursa nyingi na nzuri za kuboresha na kustawisha kiwango cha uhusiano baina ya Iran kwa upande mmoja na Tanzania na Zanzibar kwa upande mwingine.
-
Raisi: Iran ina azma kubwa ya kustawisha uhusiano na nchi za Kiafrika
Aug 06, 2021 08:00Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran na Nigeria zimekuwa zishikishirikiana vyema katika nyanja mbalimbali.
-
Sera za kigeni za serikali ya Raeisi; ushirikiano erevu na ulimwengu, mtazamo maalumu kwa majirani
Aug 06, 2021 05:20Rais wa nane wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha katika hotuba yake ya kwanza mara baada ya kuapishwa kuhusiana na utendaji wa serikali mpya ya Iran kuhusiana na sera za kigeni kwa ajili ya kudhamini maslahi ya kitaifa katika uga wa kieneo na kimataifa.