Rais Ebrahim Raisi: Daima Iran itaendelea kutetea haki za wananchi wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i73254-rais_ebrahim_raisi_daima_iran_itaendelea_kutetea_haki_za_wananchi_wa_palestina
Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, daima taifa hili litaendelea kuunga mkono na kutetea haki za wananchi wa palestina mkabala na uadui wa utawala vamizi wa Israel.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Aug 07, 2021 07:37 UTC
  • Rais Ebrahim Raisi: Daima Iran itaendelea kutetea haki za wananchi wa Palestina

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, daima taifa hili litaendelea kuunga mkono na kutetea haki za wananchi wa palestina mkabala na uadui wa utawala vamizi wa Israel.

Sayyid Raisi amesema hayo katika mazungumzo yake na Ziyad Nakhala, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina na kubainisha kwamba, hii leo ubunifu kwa ajili ya kuainisha hatima na mustakabali wa Palestina upo mikononi mwa mujahidina na makundi ya muqawama na ubunifu huu utaendelea mpaka kupatikane ushindi wa mwisho.

Rais wa Iran amesisitiza kuwa, ushindi wa mwisho ni wa Wapalestina na kwamba, kambi ya batili licha ya kumiliki silaha za kisasa lakini umeshindwa kufikia malengo yake kutokana na kusimama kidete wanamuqawama.

Rais wa Iran Ebrahim Raisi katika mazungumzo yake na Ziyad Nakhala, Katibu Mkuu wa Jihadul-Islami ya Palestina

Wakati huo huo, Rais Raeisi amesema katika mazungumzo yake na Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS kuwa, hii leo ishara za ushindi mkubwa wa mrengo wa muqawama zimejitokeza na kwamba, operesheni ya “Upanga wa Quds” ilikuwa moja ya ishara hizo.

Kuhusiana na himaya na uungaji mkono wa Iran kwa taifa la Palestina, Rais Ebrahim Raisi amesema kuwa, Tehran daima imekuwa ikiwaunga mkono wanamapambano wa Palestina na kwamba, katu taifa hili halijatetereka katika sera hizi.

Kwa mtazamo wetu, Palestina ni kadhia ya Ulimwengu wa Kiislamu, amesisitiza Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyechukua rasmi uongozi wa serikali ya awamu ya 13 baada ya kuapishwa Alkhamisi ya juzi.