Raisi: Iran ina azma kubwa ya kustawisha uhusiano na nchi za Kiafrika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i73216-raisi_iran_ina_azma_kubwa_ya_kustawisha_uhusiano_na_nchi_za_kiafrika
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran na Nigeria zimekuwa zishikishirikiana vyema katika nyanja mbalimbali.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Aug 06, 2021 08:00 UTC
  • Raisi: Iran ina azma kubwa ya kustawisha uhusiano na nchi za Kiafrika

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran na Nigeria zimekuwa zishikishirikiana vyema katika nyanja mbalimbali.

Rais Sayyid Ebrahim Raisi ameyasema hayo mapema leo katika mazungumzo yake na Zubairu Dada Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria aliyeko safarini mjini Tehran.

Amesema, kwa kuzingatia uwezo mzuri wa nchi mbili Iran iko tayari kuchukua hatua kubwa na za dhati kuboresha zaidi na kuimarisha uhusiano kati ya nchi mbili.  

Sayyid Ebrahim Raisi ameashiria namna Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilivyo na azma thabiti ya kustawisha mahusiano na nchi za Kiafrika na kuongeza kuwa: Viongozi wa Nigeria pia wanapaswa kufanye juhudi za kuondoa vizuizi vinavyoweza kukwamisha kazi ya kupanuliwa uhusiano kati ya nchi mbili.

Kwa upande wake Zubairu Dada Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria  amesema, uhusiano kati ya nchi mbili ni wa kirafiki na mzuri na kwamba anarataji kuwa kiwango cha ushirikiano wa pande mbili kitaimarishwa zaidi na zaidi katika kipindi cha sasa. 

Rais Ibrahim Raisi na ujumbe wa Nigeria mjini Tehran