-
Rais Rouhani: 1400; mwaka wa ustawi wa kiuchumi Iran na mwisho wa kipindi kizito cha vita vya kiuchumi
Mar 21, 2021 09:07Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ni jambo lisilo na shaka kwamba mwaka 1400 Hijria Shamsia utakuwa mwanzo wa ustawi mpya wa kiuchumu humu nchini na kuanza kuzaa matunda muqawama wa miaka mitatu wa taifa katika vita vya kiuchumi tulivyotwishwa na adui.
-
Ujumbe wa Nouruz wa Kiongozi Muadhamu; sisitizo la kushindwa mashinikizo ya juu ya adui na kuendelea mafanikio ya taifa la Iran
Mar 21, 2021 05:06Katika ujumbe wake wa kuwadia mwaka mpya wa Kiirani wa 1400 Hijiria Shamsia, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe wa Idi ya Nouruz kwa wananchi wa Iran na hasa kwa familia tukufu za mashahidi na majeruhi wa vita vya kujitetea kutakatifu na vilevile mataifa mengine yanayosherehekea idi hii.
-
Rouhani atoa mkono wa kheri kwa viongozi wa nchi zinazoadhimisha mwaka mpya 1400 (Nowruz)
Mar 21, 2021 00:50Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewanyooshea mkono wa kheri, baraka na fanaka viongozi na marais wenzake wa nchi kadhaa duniani ambazo zinaadhimisha sherehe za Nowruz (Nairuzi) za kuwadia mwaka mpya wa 1400 Hijria Shamsia.
-
Kiongozi Muadhamu: 1400 Hijria Shamsia ni mwaka wa "Uzalishaji, Uwezeshaji na Uondoaji Vizuizi"
Mar 20, 2021 10:58Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe maalumu kwa mnasaba wa kuingia leo mwaka wa Kiirani wa 1400 wa Hijria Shamsia na mbali na kutoa mkono wa baraka za mwaka huo mpya wa Nairuzi amesema: Mwaka huu ni wa uzalishaji, uwezeshaji na uondoaji mikwamo na vizuizi.
-
Rais Rouhani: Kusimama imara taifa la Iran kumepelekea kushindwa maadui
Mar 20, 2021 10:55Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema leo katika ujumbe maalumu kwa mnasaba wa kuwadia mwaka mpya wa Kiirani wa 1400 Hijria Shamisa kwamba kusimama imara taifa la Iran kumepelekea kushindwa maadui.
-
Iran: Hatujapokea ujumbe wowote kutoka Marekani
Mar 20, 2021 04:49Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu haijapokea ujumbe wowote kutoka kwa Marekani wala haina azma yoyote ya kuitumia Washington ujumbe.
-
Iran yatoa mkono wa pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais Magufuli
Mar 20, 2021 01:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za mkono wa pole kwa wananchi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli.
-
Qalibaf: Ni lazima Marekani iondoe vikwazo vyote dhidi ya Iran
Mar 19, 2021 08:48Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema: "Marekani inapaswa kuondoa vikwazo vyote ili Iran iweze kutekeleza ahadi zake katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA."
-
Khatibzadeh: Saudia imeliteka nyara Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi
Mar 19, 2021 04:35Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran usiku wa kuamkia leo amejibu taarifa ya mwisho ya kikao cha hivi karibuni cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi na kusema kuwa utawala wa kiimla wa Saudi Arabia umeliteka nyara baraza hilo na unachochea chuki na machafuko katika eneo hili kupitia kutwisha kwake misimamo yake isiyokubalika.
-
Nguvu za SEPAH za kukabiliana na Marekani na Israel zinaongezeka siku baada ya siku
Mar 18, 2021 23:22Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, jeshi hilo limejikita kwenye kuongeza nguvu zake za kukabiliana na mikakati ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.